MKURUGENZI wa Idara ya Maendeleo ya Filamu kutoka Bodi ya Filamu Emmanuel Ndumukwa,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Kikao cha Wadau wa Filamu na Bodi ya Filamu chenye lengo la ukusanyaji wa Filamu kwa ajili ya Tuzo za Filamu Msimu wa Pili kwa mwaka 2022 kilichofanyika leo Oktoba 23, 2022 katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


AFISA Hakimiliki Bw.Yusuph Chimbongwe,akizungumza mara baada ya Kikao cha Wadau wa Filamu na Bodi ya Filamu chenye lengo la ukusanyaji wa Filamu kwa ajili ya Tuzo za Filamu Msimu wa Pili kwa mwaka 2022 kilichofanyika leo Oktoba 23, 2022 katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Dodoma (TDFAA) Samm Kasim Takadiri,akiipongeza Bodi ya Filamu kwa kuendelea na uratibu huo wa Tuzo za Filamu kwa msimu wa pili.


Mdau wa Filamu Dodoma Pundensiana Masimo,akiipongeza bodi ya Filamu kwa kuendelea kuwakumbuka wasanii wa chini wakati wa Kikao cha Wadau wa Filamu na Bodi ya Filamu chenye lengo la ukusanyaji wa Filamu kwa ajili ya Tuzo za Filamu Msimu wa Pili kwa mwaka 2022 kilichofanyika leo Oktoba 23, 2022 katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


Muigizaji wa Filamu Dodoma Sharray Mohammed,akizungumza wakati wa Kikao cha Wadau wa Filamu na Bodi ya Filamu chenye lengo la ukusanyaji wa Filamu kwa ajili ya Tuzo za Filamu Msimu wa Pili kwa mwaka 2022 kilichofanyika leo Oktoba 23, 2022 katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


Wadau wa Filamu na Bodi ya Filamu wakiendelea na kikao cha ukusanyaji wa Filamu kwa ajili ya Tuzo za Filamu Msimu wa Pili kwa mwaka 2022 kilichofanyika leo Oktoba 23, 2022 katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

....................................

Na Alex Sonna-DODOMA

MKURUGENZI wa Idara ya Maendeleo ya Filamu kutoka Bodi ya Filamu Emmanuel Ndumukwa ametoa wito kwa Viongozi wa Wadau wa Filamu kuandaa mpango mahususi utakaowezesha Bodi kutembelea Wadau katika maeneo yao ili kuibua vipaji vipya vya Filamu na uigizaji.

Ameyasema hayo wakati wa Kikao cha Wadau wa Filamu na Bodi ya Filamu leo Oktoba 23, 2022 katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

Kikao kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya tasnia ya Filamu ikiwemo fursa na maoni ya namna bora ya kuboresha kazi za Filamu ili ziongeze wigo wa masoko na kipato kitakachowanufaisha Wadau na Jamii kwa ujumla.

“Lengo la kuwafikia Wadau mpaka ngazi ya mtaa ni kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuimarisha na kuendeleza Sanaa katika tasnia ya Filamu kwa kuibua Vipaji vipya vilivyopo maeneo mbalimbali ya Mitaa yetu,” amesema Ndumukwa

Bodi ya Filamu imeendelea na ukusanyaji wa Filamu kwaajili ya Tuzo za Filamu Msimu wa Pili kwa mwaka 2022. Ambapo wadau wa Filamu wamewasilisha kazi zao kupitia Kamati ya Tuzo iliyokuwa na Kituo cha ukusanyaji katika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.

Aidha, ukusanyaji huo wa Filamu unaendelea kupitia Mfumo wa Kidijitali kwa anuwani ya info.taffa pamoja na uwasilishaji wa Filamu kupitia Maafisa Utamaduni wa Mikoa. Ukusanyaji uliofunguliwa rasmi Septemba 30, 2022 hadi kufikia Oktoba 30, 2022.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Dodoma (TDFAA) Samm Kasim Takadiri ameishukuru Bodi kwa kuendelea na uratibu huo wa Tuzo za Filamu kwa msimu wa pili na kutoa wito kwa Wadau kuendelea kuitumia fursa hiyo kukuza na kupanua wigo na fursa za masoko.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: