Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamuwa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo akizungumza leo kwenye Kongamano la Uwekezaji na Biashara Mkoani Pwani lilifanyika kwenye Shule ya Siasa ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha Mkoani Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge akifafanua jambo kwenye Kongamano hilo la Uwekezaji na Biashara ambalo limefanyika kwenye shule ya siasa ya Mwalimu Nyerere.
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji ambaye pia ni kaimu Mkuu wa Wilaya Kibiti Meja Edward Gowele akizungumza na waandishi hawapo pichani kuhusu fursa za uwekezaji Kibiti na Rufiji
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mafia Juma Salum akielezea fursa mbalimbali za uwekezaji Wilayani humo
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya Mkuranga Khadija Nassir akiwa na Mkuu wa Wilaya Mafia Mhandisi Martin Ntemo wakiwa kwenye Kongamano hilo.
Mkurugenzi wa Kongani ya SINO TAN Juan Huan akizungumza na waandishi wa habari.
Na Khadija Kalili, Kibaha
SERIKALI imezitaka Taasisi zake wezeshi kuacha urasimu na vikwazo katika utoaji wa vibali kwa wawekezaji waliotia nia ya kuwekeza nchini ili kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan aliyeitangaza na kuijenga nchi kidiplomasia duniani katika kuvutia uwekezaji nchini.
Yamesemwa hayo leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye kongamano ambalo limewakutanisha wafanyabiashara wataalamu wa uwekezaji.
"Wawekezaji Mkoani hapa wamefanya mapinduzi makubwa ambayo yamefanyika nchini ikiwemo ujenzi wa miundombinu miradi kimkakati ni ishara ya vivutio kwa wawekezaji nchini".
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amesema hali yauwekezaji Mkoani Pwani ni nzuri kwa ulinzi na usalama huku akisema kuwa kauli mbiu inasema Pwani sehemu sahihi kwa uwekezaji.
RC Kunenge amewaomba watendaji wa serikali kusaidiana na kumsaidia Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano katika kuitangaza nchi na kuondoa vikwazo kwa wawekezaji kwa kurahisisha hatua mbalimbali za uwekezaji na kusema kuwa Mkoa wa Pwani una Kongani 23 za uwekezaji.
Aidha Waziri Jafo amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani awapongeza sana kwa suala zima la kuvutia wawekezaji ndani ya Mkoa wa Pwani, nawashukuru kwa kuunganisha mikoa ya Mtwara,Morogoro,Tanga na Lindi. kuwa mmefanya jambo kubwa na lenye tija kwa taifa zima"amesema Dkt. Jafo.
"Ikumbukwe kuwa Mheshimiwa Rais yeye ndiyo mwezeshaji mkubwa katika kuvutia wawekezaji kuja nchini na diplomasia kubwa a?meijenga duniani hivyo hatuna budi kumpongeza na kumshukuru kwa kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini Tanzania" amesema Dkt. Jafo.
"Nakupongeza sana Mkuu wa Mkoa kwa sababu nakufahamu wewe ni mchapakazi unavionjo vyote vya siasa na uongozi hivyo sina mashaka na wewe ndani ya Mkoa wa Pwani" amesema Dkt.Jafo.
Hivi sasa Pwani ndiyo Mkoa unaoongoza kwa uwekezaji nchini huku wawekezaji wengi wanaweza kupata fursa ya kuwekeza mkoani hapa na jambo la kuwatembeza watu katika maeneo mbalimbali ya uwekezaji ili waweze kuvutiwa zaidi amesema Waziri Jafo.
"Nchi yetu tuna kila sababu ya kuwa nchi ya mfano duniani katika uwekezaji kwani mapinduzi makubwa yamefanyika ndani ya nchi mfano ni ujenzi wa miundombinu katika sehemu hakuna greda lililolala nchi imeunganishwa na barabara hii ni ishara tosha kwa mwekezaji yeyote anayekuja nchini hana hofu ya usafirishaji wa bidhaa zake ndani na nje ya nchi" amesema Dkt.Jafo.
Pia nawaomba sana wawekezaji kuwa niwatoe hofu ya usafirishaji wa bidhaa zao kwani ujenzi wa njia ya kisasa ya reli kazi inaendelea ambapo itaunganisha Dar Es Salaam, Burundi na Rwanda pamoja na nchi zingine kwa ujumla.
Tanzania ni nchi iliyojipanga kimkakati kwa sababu hakuna haja ya hofu kwa wawekezaji waliopo na kwa wale ambao watavutiwa kuja kuwekeza katika nyanja mbalimbali ikiwemo ,kilimo.na uzalishaji wa pembejeo za kilimo na aina nyinginezo za uwekezaji.
Pia ninapenda kukuomba Mkuu wa Mkoa kuchagiza katika uchumi wa buluu tuna eneo kubwa la bahari Wilayani Mafia, huku nikisisitiza kwa kusema kuwa Mkoa wa Pwani ni rafiki kwa uwekezaji nchini.
Siyo mbaya ikiwapendeza Wizara ya Viwanda na Biashara kuamu maonesho ya Viwanda na Biashara ikafanyika Mkoani Pwani kwa hapa pamejitosheleza,amesema Waziri Jafo.
Watendaji wa serikali badilikeni na kuacha kabisa kuwachelewesha wawekezaji wenye nia ya kuwekeza nchini.
Kongani hizi za biashara zijengwe kisasa zaidi ili kuweza kuvutia wawekezaji kwani nchi imejipanga na uko imara katika suala la usalama wa raia na wawekezaji kwa ujumla.
Binafsi niwaombe tumepata fursa ya kuanzisha bandari kavu ya kwa kwala hivyo itasaidia sana katika kupakia na kupakua mizigo ya bidhaa za wawekezaji".
Mheshimiwa Jafo amesema hayo leo alipokuwa mgeni rasmiu kwenye kongamano la uwekezaji na biashara Mkoa wa Pwani huku akisisitiza wenye viwanda waliowekeza ndani ya mkoa wa Pwani kufungua ofisi na kujisajili Mkoani hapa ili kuweza kupandisha makusanyo ya ushuru wa Mkoa wa Pwani.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt.Selemani Said Jafo Amewataka watendaji
Watendaji wa Serikali kubadika na kuacha kabisa kuwachelewesha wawekezaji wenye nia ya kuwekeza nchini.
"Kongani hizi za biashara zijengwe kisasa zaidi ili kuweza kuvutia wawekezaji kwani nchi imejipanga na iko imara katika suala la usalama wa raia na wawekezaji kwa ujumla"amesema Jafo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge amewaomba watendaji wa serikali kusaidiana na kumsaidia Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano katika kuitangaza nchi na kuondoa vikwazo kwa wawekezaji kwa kurahisisha hatua mbalimbali za uwekezaji huku akisema kuwa Mkoa wa Pwani una Kongani 23
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji ambaye pia anakaimu Wilaya ya Kibiti Kanali Edward Gowele ameseka kuwa kwa upande wake Wilaya zake zimeandaa mazingira mazuri ya uwekezaji ambapo tayari wanawawekezaji wa kilimo cha mpunga ,miwa na uzalishaji wa sukari ambao ni Lake Agro Group pia wamepokea maombi ya uwekezaji kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa nchini ambao ni Mohammed Enterptises na Salim Said Bakhresa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mafia Juma Salum amesema anakaribisha wawekezaji katika michezo ya baharini ambapo wanajivunia kuwa na samaki mkubwa barani Afrika Papapotwe ambaye huonekana kwa msimu huku wale ambao wanaweza kuogelea hucheza nao kwenye maji (bahari) kwa sababu samaki huyu anasifa ya upole ambapo kwa kupitia samaki huyu tunapokea wageni zaidi ya 5,000 pia hatujapata namna nzuri ya kumtangaza kiutalii duniani kote lakini tunaimani kubwa kwa kupitia filamu ya Royal Tour atatangazika na kuingizia Halmashauri kipato, amesema Mkurugenzi huyo wa Mafia.
Kongamano hilo limehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas, wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Pwani Wakurugenzi na Wenyeviti wa Halmashauri zote, wataalamu wa masuala mbalimbali wote wakikadiriwa kuwa 196 ikiwa ni kati ya washiriki 250 ambao walikusudiwa kuwepo kwenye kongamano hilo.
Post A Comment: