Na Zanura Mollel, LONGIDO


Naibu Waziri wa Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Longido Dkt Steven Kiruswa amesema anasikitishwa na Siasa za Ukanda ,Urika na Ukabila unaoendelea wilayani hapo na kupelekea mgawanyiko kwa wananchi wa eneo hilo.


Alisema hayo kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya kichama Longido,ambapo aliahidi baada ya chaguzi hizo amejiapanga kuandaa semina kwa viongozi wa Chama hicho lengo ikiwa ni kuvunja makundi hayo yanayodaiwa kuwepo.


" Mategemeo yangu baada ya uchaguzi  ni kuwa wa moja na kuachana na makundi,na Mimi na ahidi kushirikiana na atakaye shinda kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Chama wilaya wote ni wangu Sina ninaye mpambania aweze kushinda" alisema Dkt Kiruswa.


Mgombea Papa Nakuta aliahidi kuhakikisha ujenzi wa ofisi ya Chama hicho unakamilika kwa wakati lakini pia alieleza kuhakikisha kuongezwa kwa matawi ya Chama hicho katika maeneo yenye upungufu wa matawi ikiwemo tarafa ya Enduiment yenye kata nne ikidaiwa kuwa na matawi 12.


Joseph Ole Sadira ni mgombea na ndiye Mwenyekiti aliyekua madarakani kwa miaka mitano,akitetea kiti chake alisema alipoingia madarakani alipambana kudhohofisha uponzani kwa kuwarejesha madiwani ndani ya Chama hicho,Kuomba ongezeko la matawi pamoja na kamalizia ujenzi wa ofisi ya Chama.


Joel Maumba alisema endapo atapata nafasi hiyo atahakikisha wanachama wa Chama hicho wanakua wamoja,na kaliza mpasuko na mgawanyiko uliopo ndani ya Chama hicho wilayani hapo.


Chama kimerejesha majina matatu ya wagombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilayani hapo ambao ni Papa Nakuta,Joseph Ole Sadira na Joel Maumba.


Mwisho.

Share To:

Post A Comment: