Na Fredy Mgunda, Iringa.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga amewataka kuwa wakurugenzi wa maisha yako kutokana na kutumia vijapaji walivyonavyo kwa kuzingatia muda na matumizi mazuri ya fedha walizonazo.
Akizungumza kwenye kipindi cha Morning Talk cha radio Ebony fm iliyopo mkoa Iringa,mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga alisema kuwa hakuna serikali duniani inayoweza kuajili vijana wote hivyo vijana inatakiwa kujiajiri wenyewe kwa kuwa na nidhamu ya fedha unazopata.
Kiswaga alisema kuwa mawazo mengi ya vijana ni kuajili na serikali jambo ambalo sio la kweli,vijana wanatakiwa kujituma, kuwawabunifu na kufanya kazi kwa kujituma na uaminifu hapo ndio utakuwa mkurugenzi wa maisha yao.
Alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wavivu kufanya kazi ndio maana unaona kwa mwaka mzima unakuta vijana wametumia miezi miwili au mitatu kuzalisha kati ya miezi kumi na mbili jambo ambalo linawafanya vijana kukimbilia kuajili serikalini.
Kiswaga alisema kuwa kijana akifanya kazi kwa masaa nane kwa siku na kwa mwaka mzima na akiwa na matumizi bora ya fedha anazozipata atakuwa tajili na mkurugenzi wa maisha yake.
Alisema kuwa vijana wengi wanatumia kiasi kikubwa cha fedha tofauti na uzalishaji wake,wanatumia miezi miwili au mitatu kuzalisha lakini wanatumia fedha hizo kwa miezi nane hivyo hapo lazima utaona vijana wanalalamika kila wakati.
Kiswaga alisema kuwa matajili wengi duniani ni wananchi ambao walianza kujiajiri toka wakiwa vijana kwa kuwa na nidhamu ya kazi, matumizi bora ya muda na fedha ambazo anakuwa anazizalisha kwa wakati huo
Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga alimazia kwa kuwataka vijana kuacha kukata tamaa mapema pale wanapokutana na vikwanzo vya kimaendeleo lazima kutumia maarifa,ubunifu na kuongeza nidhamu ya kazi.
Post A Comment: