YUSUPH Bujiku ameibuka kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Ilemela.
Msimamizi mkuu wa uchaguzi huo, Wilaya ya Ilemela, Simon Mangelepa, alimtangaza Yusuph Bujiku kuwa mshindi, baada ya kupata kura 485 na mpinzani wake Suzana Kabula, kupata kura 279, huku Angelina Josephat alipata kura 13 kati ya kura 777.
Mangelepa ametangaza matokeo hayo usiku wa kuamkia leo, wakati wa uchaguzi wa chama hicho uliofanyika ukumbi wa Winterfalls katika kata ya Nyasaka mkoani Mwanza.
Akizungumza baada ya matokeo, Bujiku alisema uchaguzi wa chama chao ngazi ya wilaya umeisha na ni wakati wa kukijenga chama chao.
‘’Shukran zangu za dhati kwa wanachama wa CCM Wilaya ya Ilemela kwa kunichagua. Hakika mmeonesha imani kubwa sana kwangu, ninachoomba kwa sasa ni ushirikiano wenu,’’ amesema Bujiku.
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela, Aziza Isimbula amewaomba viongozi wapya wa chama hicho katika ngazi ya wilaya kuendelea kusimamia na kutekeleza ilani ya chama chao.
Post A Comment: