Na Christina Thomas; Morogoro
Basi la kampuni ya BM imegonga na kuua Mtu mmoja alie fahamika kwa jina moja la Alfonsi katika ajali iliyotokea eneo la Makunganya Manispaa ya Morogoro mara baada ya gari yake ndogo aina ya Nissan Mitsubishi yenye namba za usajili T 847 CWN iliyokuwa ikitokea Morogoro kuelekea Dodoma kugongwa kwa nyuma na basi ya kampuni ya BM iliyokuwa ikitokea Dar Es Salaam kuelekea Turiani wilayani Mvomero yenye namba za usajili T 959 DDE iliyokuwa na Abiria 33 .
Mkaguzi msaidizi jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Morogoro Ahmed Lemba amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kusimama ghafla kwa Lori lililokuwa mbele ya gari ndogo na kupelekea gari ndogo kugonga lori hilo na kugongwa kwa nyuma na basi ya BM Couch lililokuwa nyuma yake.
Nae dereva msaidizi wa basi la kampuni ya BM Couch Saidi Ally amesema kuwa lori lililokuwa mbele ya gari ndogo lilisimama ghafla na kufanya gari za nyuma zishindwe pakupita hivyo kupelekea gari ndogo kugonga lori na lenyewe kugongwa na basi na kuingia chini ya lori .
Post A Comment: