Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa Kijiji cha Mwamakalanga katika halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, ameachwa akiwa na ulemavu wa kudumu baada ya kung’atwa kipande cha ulimi wake, na mwanamke anayesadikiwa kuwa na mahusiano naye ya kimapenzi.
Kwa mujibu wa Kaka wa majeruhi , mtuhumiwa anayejulikana kwa jina la Leticia Elias mwenye umri wa miaka 40, alimwita mdogo wake nyumbani kwake kwa lengo la kufanya mazungumzo, lakini baadaye walianza kufanya tendo la ndoa na kumtaka aingize ulimi kwenye mdomo wake (wanyonyane ndimi) na ndipo akatumia nafasi hiyo kumng’ata kipande chake cha ulimi.
Kufuatia tukio hilo, Kaka huyo wa majeruhi ameimbia Redio Faraja kuwa, hali ya ndugu yake bado siyo ya kuridhisha kutokana na kidonda alichobaki nacho kwenye sehemu ya ulimi iliyobaki, na hawezi kula kwa njia ya kawaida licha ya kupatiwa matibabu na kuruhusiwa, baada ya kupewa dawa ya kutumia katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwamakalanga James Jidayi, amekiri kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa, limetokea Septemba 29 Mwaka huu majira ya saa tatu usiku, ambapo alipata taarifa kupitia kwa mtendaji wa kijiji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi, amethibitisha kupokea taarifa za tukio hilo na kubainisha kuwa, wanaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo.
Post A Comment: