MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Mkoani Tanga Audrey Claudius akizungumza wakati wa wiki ya huduma kwa wateja 
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Mkoani Tanga Audrey Claudius akizungumza wakati wa wiki ya huduma kwa wateja 
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Mkoani Tanga Audrey Claudius akionyesha 

,Afisa Mkuu  NSSF Mkoa wa Tanga,Abubakari Mshangama  kushoto akimuelekeza jambo mmoja wa wanachama wa mfuko huo 

,Afisa Mkuu  NSSF Mkoa wa Tanga,Abubakari Mshangama  kushoto akimuelekeza jambo mmoja wa wanachama wa mfuko huo 


Na Oscar Assenga,TANGA

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii nchini (NSSF)  wameadhimisha siku ya wateja duniani huku wakiwataka waajiri mkoani Tanga kuhakikisha wakati wanalipa michango yao kwa kutumia mifumo ya kieletroniki ili kurahirisha mwanachama aweze kulipwa papo kwa papo.


Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko huo mkoani Tanga Audrey Claudius wakati akizungumza kwenye wiki ya huduma kwa wateja  iliyofanyika kwenye ofisi zao Jijijni Tanga 

Meneja huyo alisema lazima taarifa za mwanachama ziwe kamilifu ndio maana wanasisitiza waajiri kuanzia sasa kutumia mfumo huo ambao utawezesha mnufaika kuweka kulipwa kwa wakati. 

Alisema katika wiki hii watahakikisha wanachama wote wanaowadai watawalipwa ndani ya siku moja huku aliwataka waajiri wawawasaidie kulipa michango kwa kufuata mifumo na walipe kila mwezi. 

"Lakini pia niwatake waajiri  kuacha kulimbukiza michango kwani kufanya hivyo kunasababisha usumbufu kwa wanachama wanapo kwenda kufungua madai hivyo tuhakikishe tunalipa kwa wakati"Alisema Meneja huyo 

Hata hivyo aliwataka waajiri mkoa wa Tanga kuhakikisha wanalipa michango yao  na wenye malimbikizo wamepewa mikataba ya namna ya kulipa michango huku akiwasisitizia walipe kufuatana na mikataba waliopewa.

Awali akizungumza ,Afisa Mkuu  NSSF Mkoa wa Tanga,Abubakari Mshangama alisema katika wiki ya huduma kwa wateja wameweza kutoa huduma mbalimbali ikiwemo ya huduma ya mtandao ambao utawawezesha wanachama hao kuweza kupata taarifa zao.

Mshangama alisema kwa waajiri wanaweza kutumia member portal hiyo wanaweza kuwasiji wanachama na kulipa michango yao ikiwemo kupata taarifa mbalimbali za Shirika hilo.

Aidha alisema wiki hii wanatoa elimu zaidi kuhusu huduma hizo za kimtandao huku akiwataka wananchi kujiunga na Shirika hilo ili kuweza kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa

Naye kwa upande wake mwanachama wa Mfuko huo Modo Mkufya alisema Mfuko huo wanaiomba Serikali waboreshewe pensheni hizo kidogo.

Awali naye Catharine Ramadhani alisema wamefurahi kushiriki kwenye wiki hiyo huku n
akiomba huduma ziboreshwe ikwemo kuhakikisha wanaondoa vikwazo ambavyo vimekuwa vikijitokeza awali.

Alisema kwamba huduma za Mfuko huo ni nzuri huku akiwataka wananchi wengine wajiunga nao ili kuweza kunufaika na mafao mbalimbali.

Hata hivyo kwa upande wake Raphael Maguzo ambaye ni Mstaafu alisema wanafurahishwa na huduma ambazo zimekuwa zikitolewa na Mfuko huo maana aliweza kufungua madai ambao yalifanyiwa kazi kwa wakati.



Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: