Waziri wa kilimo Hussein Bashe akizungumza leo jijini Dodoma katika kikao maalumu cha Wizara ya Kilimo, Tamisemi na wakuu wa mikoa kote Nchini leo jijini Dodoma.
Na Janeth Raphael
SERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo imesema kuwa katika kuhakikisha Bodi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Kilimo zinafanya kazi kwa ufanisi na wenye tija kwa wananchi na zao husika itawateua Wakuu wa Mikoa kutoka kanda ya mazao mbalimbali nchini kuwa wajumbe wa bodi ili kufanikisha malengo na juhudi za Kilimo nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo, Mh. Hussein Bashe leo jijini Dodoma katika kikao Maalum cha Wizara ya Kilimo, Tamisemi na Wakuu wa Mikoa kote nchini ambapo amesema kuwa Bodi ndio sehemu pekee inayotengeneza mipango,malengo na dira ya zao husika.
"Sasa tunateua watu ili wakaongeze nguvu ya kuimarisha zao husika katika maeneo yao, Rais Samia suluhu Hassan alivyoteua Wayeviti wa Bodi niliamua kuteua wakuu wa mikoa kidogo kumekuwa na mjadala kuhusu hili lakini mawazo yangu nimakubwa mno katika sekta ya kilimo nchini, nasiwezi kuteua bodi ya pamba sina mkuu wa Mkoa au Mkuu wa wilaya anayehusika na pamba au zao flani" Amesema Waziri Bashe.
Kwa upande wake waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), innocent Bashungwa amesema Ruzuku ya Mbolea ni dhamira ya Rais samia suluhu Hassan kuwasaidia wakulima ili wazalishe kwa Tija kwa Maslahi yao mwenyewe na Taifa kwa ujumla.
"Rais samia suluhu Hassan ametoa Ruzuku hii kwa wakulima ili kuwasaidia lakini tunaona nchi zingine zikiwaacha wakulima wanapambana na hali zao lakini Rais Samia akasema hapana lazma niwasaidie wakulima wangu" Amesema innocent Bashungwa.
Akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Ruzuku ya Mbolea kwa Msimu wa Mwaka 2022/2023,Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania(TFRA) Dkt. Stephan Ngailo amesema kutokana na kupanda kwa bei za Mbolea katika soko la dunia serikali ya Tanzania imetenga kiasi cha shilling Billion 150 kugharamia Ruzuku ya Mbolea ili kuongeza uzalishaji na Tija katika kilimo.
"Mpango wa Ruzuku kwa Mwaka 2022/2023 ni kupunguza gharama ya Mbolea, kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, kuimarisha usalama wa chakula na kuongeza upatikanaji wa Malighafi za Viwanda vya Ndani" Amesema Dkt.Stephan Ngailo.
Dhima ya Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ni Kuhakikisha upatikanaji wa mbolea bora na bei rahisi kwa Wakulima wote kwa kusimamia tasnia ya mbolea ili kuleta uzalishaji endelevu katika kilimo.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashunguwa akizungumza leo jijini Dodoma katika kikao maalumu cha Wizara ya Kilimo, Tamisemi na wakuu wa mikoa kote Nchini Dodoma.
Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA) Dkt Stephan Ngailo akizungumza leo jijini Dodoma katika kikao maalumu cha Wizara ya Kilimo, Tamisemi na wakuu wa mikoa kote Nchini leo jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakiwa katika mkutano huo.
Post A Comment: