Mtoto Carlen Stephen (kulia) akiongoza ibada ya watoto katika Sikukuu ya Watoto wa Kanisa la Moravian Tanzania Usharika wa Sabasaba mkoani Singida iliyofanyika Septemba, 25, 2022. Kushoto ni Mwalimu wa watoto hao, Celina Mpaki.
Mtoto Samuel Mwanitu akisoma neno la Mungu kwenye ibada hiyo.
Mtoto Winfrida Edward Mdaki akisoma matangazo wakati wa ibada hiyo.
Mtoto Lillian Lugano akiwatangaza watoto waliofanya vizuri mtihani.
Mwalimu wa Watoto hao, Jemina Kalinga akizungumza.
Mwenyekiti wa Wanawake wa kanisa hilo, Agnes Mwaihojo akichangia jambo kwenye sherehe hiyo.
Watoto wakiwa wamejipanga tayari kwa kuingia kanisani kuanza ibada hiyo.
Mchungaji wa kanisa hilo, Oscar Falanga (wa pili kulia) na Mzee wa kanisa hilo  Obedi Mwalwiba (kulia) wakiongoza watoto hao kuingia kanisani.
Watoto wakiingia kanisani.
Watoto wakiimba wimbo maalumu wa sherehe hiyo.
Waumini wakiwa kwenye ibada hiyo.
Ibada ikiendelea.
Mzee wa kanisa hilo Obedi Mwalwiba akizungumza.
Mchungaji wa kanisa hilo, Oscar Falanga akiungumza.
Watoto wakitoa burudani wakati wa sherehe hiyo.
Muchungaji wa kanisa hilo Oscar Falanga akitoa zawadi kwa mtoto, Samwel Mwanitu mmoja wa watoto  waliofanya vizuri mtihani.
Zawadi ikitolewa kwa Winfrida Edward.
Zawadi ikitolewa kwa mtoto Hamphray Albert Kasoga.
Zawadi ikitolewa kwa Brightnes Israel..
Zawadi ikitolewa kwa Carlen Stephen.
Walimu wa watoto hao wakiwa na zawadi zao baada ya kukabidhiwa. Kutoka kushoto ni Mwalimu wa watoto hao, Jemina Kalinga, Celina Mpaki, Bwigane Mwalwiba na Lillian Lugano.
Furaha ikitamalaki baada ya kupokea zawadi zao. 
 

 Na Dotto Mwaibale, Singida


WATOTO wa Kanisa la Moravian Tanzania Usharika wa Sabasaba Mkoa wa Singida, wameliombea taifa na viongozi wake wote huku wakiwahimiza wazazi kuendelea kuwapa malezi na matunzo bora.

Wameyasema hayo kwenye Sikukuu yao iliyofanyika katika Kanisa la Moravian Usharika wa Sabasaba mjini hapa sherehe ambayo inafanyika katika makanisa yote ya Moravian hapa nchini kwa utaratibu uliowekwa na kanisa hilo.

Katika ibada ya sherehe yao hiyo watoto hao walimuombea Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri, Wabunge,Spika wa Bunge,  Wakuu wa Mikoa na wilaya , Makatibu wakuu na viongozi mbalimbali ili Mungu aendelee kuwapa afya njema na  kutumikia Serikali.

Watoto hao mbali ya kufanya maombi hayo walitumia nafasi hiyo kuwaomba walezi na wazazi wao kuendelea kuwatunza na kuwapa malezi bora kwa kuwapa chakula, malazi, mavazi,kuwapeleka shuleni na kanisani ili wakue kiroho, maarifa  na kiimani.

"Tunawaomba wazazi wetu wawe wanawaruhusu  kuja kanisa ambako tunakutana watoto wote kujifunza mambo mbalimbali na neno la Mungu ili tukue katika imani na kiroho na kuwa watoto bora" alisema Samuel Mwanitu.

Mwanitu alisema kutoa baraka kwa watoto ni jambo jema kwani ndio watakuwa viongozi wajao na akaongeza kuwa Yesu  alisema waacheni watoto wadogo waende kwake naye aliwakumbatia na kuwabariki.

Watoto hao katika ibada hiyo walioiongoza waliweza kufanya burudani kwa kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, kusoma vifungu kadhaa vya baadhi ya maneno kutoka kwenye biblia na kutoa zawadi kwa watoto wenzao waliofanya mitihani ya kanisa,  zawadi ambazo zilitolewa na mchungaji wa kanisa hilo Oscar Falanga huku muumini wa kanisa hilo Agnes Mwaihojo akiwazawadia walimu wa watoto hao zawadi kutokana na kujitoa kwao kuwafundisha. 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: