TAKRIBANI wananchi 1,000 wilayani Missenyi, tayari wameunganishwa bure na huduma za maji, baada ya kukamilika kwa mradi wa maji Kyaka-Bunazi.
Mradi huo unaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mwanza (Mwauwasa), ulizinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan mapema mwezi Juni mwaka huu.
Msimamizi wa mradi, Mhandisi Nuhu Msuya, amesema leo kwamba wakazi waliounganishwa bure ni wazee, watu wenye ulemavu pamoja na waliothibitika kutokua na uwezo wa kumudu gharama za uunganishwaji.
“Hawa tayari wamelipiwa na serikali kila kitu na ni wale walio jirani na inapopita miundombinu ya mradi. Lakini watakuwa wakilipia ankara za maji,” amesema.
Katika hatua nyingine amesema zaidi ya wateja 600, zikiwemo taasisi, tayari wamewasilisha maombi na shughuliza za kuwaunganisha na huduma zinaendelea.
Sambamba na hilo, huduma hiyo pia inawafikia wananchi kwa ujumla kupitia vituo maalum vya kuchotea maji, vilivyojengwa kama sehemu ya mradi huo.
Post A Comment: