Akitoa maagizo hayo wakati wa ziara ya Bodi ya Ushauri ya TARURA katika Mkoa wa Kilimajaro, Mhandisi Seff alisema kuwa ni lazima barabara hiyo ikamilike ikiwa ni pamoja na kuweka alama za barabarani kama ilivyoainishwa kwenye mkataba.
“Sehemu ya kwanza nimeambiwa imekamilika na ipo katika kipindi cha matazamio lakii sehemu ya pili ipo asilimia 52 na nimeambiwa kulikuwa na changamoto za malighafi. Sasa kwakuwa changamoto hizo zimekwisha, nawaagiza kuhakikisha barabara hii iwe imekamilika ifikapo katikati ya mwezi huu wa tisa,” alisema Mhandisi Seff.
Kwa upande wake Mhandisi Nicolas Francis, meneja wa TARURA Mkoa wa Kilimanjaro alisema kuwa wameepokea maelekezo na watahakikisha wanayatekeleza ili mradi ukamilike kwa wakati na kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.
“Tumesisitizwa pia kuhakikisha tunaweka alama za barabrani ili kuimarisha usalama katika barabara zetu, tutalikamilisha hilo mara baada ya barabara kukamilika kwa sababu katika dhima nzima ya kutengeneza barabara, usalama lazima uwe kipaumbele,” alisema mhandisi Nicolas.
Aidha bodi ya ushauri ya TARURA katika ziara hiyo walitembelea barabara ya utafiti ya lawati - kibongóto katika maeneo ya mashamba Sanyajuu na kuagiza TARURA wilaya kuzitunza barabara hizo kwa kuzifanyia ukarabati ili ziweze kudumu na kuwasaidia wananchi.
Post A Comment: