Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu Kongamano la Fursa za Kibiashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo tarehe 26 Septemba, 2022 jijini Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu Kongamano la Fursa za Kibiashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo tarehe 26 Septemba, 2022 jijini Dar es Salaam. Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Nchini Tanzania, Bw. Kanupangi Yamba Gilbert akuzungumza wakati wa mkutano na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu Kongamano la Fursa za Kibiashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo tarehe 26 Septemba, 2022 jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
****************************
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema Tanzania inatarajia kuiunganisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Mkongo wa Taifa ili kuipatia huduma ya Internet.
Waziri Nape amebainisha hayo leo Septemba 26, 2022 jijini Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kongamano la Biashara baina ya Tanzania na DR Congo litakalofanyika Oktoba 18 hadi 19 mwaka huu kwa lengo la kukuza matumizi ya TEHAMA.
“Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itakuwa ni nchi ya nane kuunganishwa na Mkongo wa Taifa kwani kwa sasa tumeshauunganisha kwa nchi saba,” amesema Nape.
Akizungumzia Kongamano hilo amesema moja ya mkakati wa Serikali ya Tanzania ni kuhakikisha inaongeza matumizi ya TEHAMA kwa kuweka mazingira wezeshi ya kisera na Sheria.
Vile vile amesema ili kufanikisha hilo ni lazima kushirikiana na Sekta binafsi katika kuimarisha miundombinu ya TEHAMA na Mawasiliano.
Waziri Nape amesema kwamba Kongamano hilo litahudhuriwa na washiriki 300 kutoka Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ambapo amesema kuwa watajadili namna ya kuimarisha TEHAMA.
“Lakini pia kutakuwa kutafanyika maonyesho ya bidhaa za Ubunifu wa TEHAMA. Kujadili mashirikiano ya biashara na kampuni za Kongo ili kufanya biashara pamoaj,” ameongeza Nape.
Nape pia ameeleza kuwa makampuni machanga yatapata fursa ya kuonesha na kutangaza boashara zao.
Aidha Nape amesema Kongamano hilo litafunguliwa na Waziri wa Posta na Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Congo Augustin Maliba.
Post A Comment: