Na Christina Thomas, Ulanga
WAKAZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro wanatarajia kuondokana na adha ya kukatika kwa umeme kufuatia ukarabati wa mradi wa transfoma unaogharimu zaidi ya kiasi cha shilingi Bilioni 1.9 kukamilika mapema tarehe 23 mwezi wa 11 Mwaka huu.
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro Mhandisi John Lujani amesema hayo wakati alipotembelea kituo cha kupozea umeme kilichopo Ifakara ambapo amesema baada ya mradi huo kukamilika kutasaidia kuepuka changamoto ya kukosekana umeme waliyokuwa wakiipata iliyotokana na kuungua kwa transfoma kubwa la umeme katika kituo Cha kupozea umeme Msamvu.
Alisema kukamilika kwa transfoma hiyo kutasaidia kutatua changamoto ya kukatika kwa umeme na kufanya jamii kuendelea na shughuli zao za kila siku za kukuza uchumi hasa kwa wale ambao wanaotegemea nishati ya umeme.
Naye Mbunge wa Jimbo la Ulanga Salim Hasham amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika katika Jimbo hilo na kuwezesha kufungua viwanda na vitu vingine.
“kituo kikikamilika kitasaidia katika shughuli za kukuza uchumi ikiwemo kuendelea na shughuli za uchimbaji madini pamoja na uwekezaji mwingine” alisema Hasham.
Mbunge huyo amesema kuwa mpango wa sasa wa Serikali ni kupeleka umeme katika kila kitongoji na kuhakikisha hali ya umeme inakua nzuri.
Naye Mhandisi mkazi John Mwamaso amesema kukamilika Kwa mradi kutatatua changamoto wanayo ipata wananchi mala Kwa mala ya kuungua Kwa kituo cha kupozea umeme Cha Msamvu.
Mhandisi huyo amesema mradi huo utapokea umeme kutoka vyanzo viwili cha kidatu na kuhansi ili kuisaidia Vituo vingine visilemewe.
Post A Comment: