Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Anthony Mavunde akizungumza na watu wenye ulemavu (hawapo pichani) katika uzinduzi wa mafunzo ya siku mbili (28-29 Septemba) ya kilimo biashara kwa watu wenye ulemavu ya Foundation of Disabilities Hope (FDH) na yaliyodhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti mkoani Dodoma.

 Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) imedhamini mafunzo ya siku mbili ya mafunzo ya kujiongezea kipato kupitia kilimo kwa watu wenye ulemavu katika jitihada za kuchochea ukuaji uchumi shirikishi nchini. Mafunzo hayo yameendeshwa kwa ushirikiano baina ya SBL na shirika liitwalo, Foundation of Disabilities Hope (FDH).


Mafunzo hayo yameanza tarehe 28 Septemba mjini Dodoma yakishirikisha zaidi ya watu 100 wenye ulemavu watakaopata mafunzo ya wa kilimo biashara, ujasiriamali na ujuzi wa masuala ya fedha ili kuwasaidia kuingiza kipato zaidi katika shughuli zao za kila siku za kiuchumi.

Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa SBL, John Wanyancha alisema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya dhamira yao ya kukuza kasi ya uchumi nchini Pamoja na kudumisha mpango wao wa miaka kumi ya kujenga jamii shirikishi na endelevu.

Zaidi ya hayo, John alisema, "Tunajivunia kushirikiana na FDH kuwezesha mafunzo haya ya kuwasaidia watu wenye ulemavu kuongeza mapato yao, ambapo zaidi ya watu 100 watanufaika na fursa hii. Tuna imani tutaweza kutengeneza kundi jipya la maafisa kilimo na wataalamu wa kilimo biashara na hivyo kuimarisha sekta yetu ya kilimo ambayo ndio uti wa mgongo wa uchumi wetu. ‘Pia tunatazamia kutoka kundi hili kununua malighafi yetu ya utengenezaji bia ambayo hatimaye itainua kipato chao na kuinua kiwango chao cha maisha’.

Wanyancha alielezea jinsi SBL imejitolea kushawishi wadau wengine nchini kuunga mkono jitihada za kujenga jumuiya jumuishi ambapo kila mtu, bila kujali hali yake ya kimwili, anaweza kufurahia maisha popote, wakati wowote.

Alisema, ‘tuko tayari kufanya kazi na taasisi za watu wenye ulemavu katika kila idara ili kuhakikisha tunajenga jamii uendelevu na kusaidia serikali kufikia ukuaji wa uchumi jumuishi bila kumwacha mtu yoyote nyuma’.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Athony Mvunde (Mbunge) ambae alimuwakilisha Waziri wa Kilimo, Mhe Hussein Bashe (Mbunge) alitambua kazi inayofanyika na SBL katika kusaidia kilimo nchini kupitia shughuli zake za biashara ambazo kwa wastani wananunua zaidi ya tani 18,000 za nafaka kwa mwaka kutoka kwa wakulima.

Alinukuliwa, "Tunaishukuru sana SBL kwa kuleta ustahimilivu wa kilimo katika nchi yetu kwa kujumuisha watu wenye ulemavu," alisema.

Aliendelea kusema, ‘Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, tangu aingie madarakani ameonyesha nia ya dhati ya kufanya kazi na sekta binafsi kama injini ya kukuza uchumi, hasa katika kilimo. Ndiyo maana tunajitahidi kuifanya sekta hii kuwa ya kibiashara kwa kuwavutia wawekezaji na wakulima wengi zaidi ambao wataleta mapinduzi katika sekta hii na kuchochea ukuaji wa uchumi - na kwa hili, tunaipongeza SBL kwa kuunga mkono wito wetu’.

SBL imedhamira kushirikiana na vyama vya watu wenye ulemavu na wadau mbalimbali ili kusukuma ajenda ya jamii ujumuishi katika kuendeleza jamii nzima. SBL inatambulika kupitia juhudi zingine zinazofanyika kama kupitia ufadhili wa masomo kwa watu wenye ulemavu kusomea kozi zinazohusiana na kilimo katika dirisha lao jipya la Kilimo-Viwanda Scholarship lililozinduliwa Agosti mwaka huu.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Anthony Mavunde (watatu kulia walioketi) akiwa katika uzinduzi wa mafunzo ya siku mbili (28-29 Septemba) ya kilimo biashara kwa watu wenye ulemavu ya Foundation of Disabilities Hope (FDH) na yaliyodhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti mkoani Dodoma. Wa kwanza kulia ni, Michael Salali (Mwenyekiti wa FDH), akifuatiwa na John Wanyancha (Mkurugenzi Mahusiano ya Umma wa SBL). Wa kwanza kushoto ni Neema Kweka (Muwakilishi ofisi ya Rais, TAMISEMI) na akifuatiwa na Yustina Munishi (Mkuu wa Divisheni ya kilimo mjini Dodoma). Waliosimama nyuma ni wakufunzi wa Kilimo biashara


Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Anthony Mavunde (watatu kulia walioketi) akiwa katika uzinduzi wa mafunzo ya siku mbili (28-29 Septemba) ya kilimo biashara kwa watu wenye ulemavu. Wa kwanza kulia ni, Martin Kihumbe (Mkurugenzi wa FDH), akifuatiwa na John Wanyancha (Mkurugenzi Mahusiano ya Umma wa SBL). Wa kwanza kushoto ni Neema Kweka (Muwakilishi ofisi ya Rais, TAMISEMI) na akifuatiwa na Yustina Munishi (Mkuu wa Divisheni ya kilimo mjini Dodoma).


Share To:

Post A Comment: