Na Theophilida Felician Kagera.



Jeshi la Polisi Mkoa Kagera linamshikilia mtu mmoja raia wa nchi ya Uganda kwa tuhuma za kumiliki mihuriya mamlaka za Serikali kinyume cha  sheria.



Taarifa ya kushikiliwa kwa mtu huyo  imetolewa naye kamanda wa Jeshi la Polisi  Mkoa Kagera William Mwampaghale kwa vyombo vya habari osifini kwake Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.



Kamanda huyo amesema kuwa mtuhumiwa  alikamatwa  na Jeshi hilo mnamo Tarehe 1/9/ mwaka huu huko kitongoji cha Katebe Kijiji cha Mutukula  Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera.



Ameitaja mihuri hiyo kuwa ni pamoja na muhuri wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) (KILIMO) NA (MIONZI hivyo Jeshi hilo baada ya kuhojiana naye awali alikiri  kukamatwa na mihuri hiyo na kueleza kuwa amekuwa akiitumia kugonga kwenye nyaraka bandia ambazo huzitumia kuvusha magari mbalimbali ya mizigo kwenda Nchi ya Uganda  kupitia mpaka wa Mutukula uliopo kati ya Tanzania na Uganda.

 


Amefafanua kuwa jeshi hilo kwakushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vimefanikiwa kumtia nguvuni baada kupewa taarifa za kuwepo kwa mtu huyo ambaye kazi yake ni ajenti wa mizigo katika eneo hilo  la Mtukula, hivyo mpaka kukamatwa kwake alishafanikiwa kuyavusha magari (11)  ambayo ni Fuso (9) na Semi Trailler (2).



Hata hivyo ameongeza kusema kuwa upelelezi unaendelea ili kuweza kubaini mtu huyo anashirikiana na mtandao gani wa uhalifu ndani ya vyombo vya Serikali katika kushiriki vitendo hivyo vya hujuma dhidi ya mapato ya Serikali na utakapokamilika atafikishwa mahakamani kujibu dhidi ya tuhuma hizo.



Mbali na tukio hilo ametoa wito kwa watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria  kwa kujua ama kwa kutokujua taratibu za  kisheria  katika umiliki wa silaha, wa hakikishe wanazisalimisha kwa hiyari  ndani ya muda wa kipindi cha miezi miwili  kuanzia mnamo Tarehe 5/ 9/ hadi mwishoni mwa mwezi wa October mwaka huu wa 2022, kama ilivyokwisha tangazwa na   waziri wa mambo ya ndani Mhe Hamad Yussuf Masauni. 



 Mwampaghale amewasihi wananchi kuendelea  kushirikiana na Jeshi hilo katika kutoa taarifa za kusaidia kuwabaini watu wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu huku akiapa na kuwaonya watu wa namna hiyo katu hawatabakia salama "tumejipanga kikweli kweli"amehitimisha kwa msistizo huo kamanda  William.

Share To:

Post A Comment: