Naibu Waziri wa Kilimo  Anthony Mavunde amewataka wachakataji wa mazao ya kilimo kuingia mikataba ya kilimo na wakulima nchini Tanzania ili kurahisisha upatikanaji wa masoko wa mazao ya kilimo.

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo jana  wakati wa hafla fupi ya uwasilishaji wa taarifa ya mafanikio ya Program ya Smart Agriculture inayoratibiwa na Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) iliyohusisha mazao ya mtama,shayiri na zabibu.

“Niwapongeze TBL kwa kuja na program hii ya kuwafikia wakulima wa mazo ya shayiri,mtama na zabibu kwa kuwajengea uwezo wa mafunzo ya kilimo,matumizi ya teknolojia na kuwaunganisha na huduma za kifedha.

Mfumo huu wa kilimo mkataba unaotumiwa na TBL unampa uhakika mkulima juu ya masoko ya mazao yake na hivyo kutatua changamoto kubwa ya upatikanaji wa soko la uhakika la mazao yetu.

Nitoe rai kwa kampuni nyingine ambazo zinafanya uchakataji wa mazao ya kilimo,kuiga mfano huu mzuri wa TBL wa kuingia mikataba ya kilimo na wakulima ili kuwahakikishia wakulima soko la mazao yao sambamba na kuzalisha kwa tija kupitia huduma za ugani zinazotolewa na wataalamu wa TBL kwa ushirikiano na wale wa serikali”Alisema Mavunde

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TBL  Jose Maron ameeleza juu ya mafanikio makubwa yaliyopatikana wakati wa utekelezaji wa program hii ya Smart Agriculture ambapo wakulima wamepata masoko ya uhakika ya mazao yao kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja, asilimia kubwa ya wakulima kutoka mikoa ya Manyara na Dodoma wamejengewa uwezo juu ya matumizi ya teknolojia katika kilimo chao na pia kupata gursa ya elimu ya fedha na kufikia mikopo ya kilimo kwa urahisi









Share To:

Post A Comment: