Dar es Salaam, Wawekezaji wenye nia ya kuwekeza, wamealikwa kutumia fursa katika mradi mpya wa kiuchumi wa Mkinga, mradi huo wa mamilioni ya dola utaipeleka Tanzania katika kilele kipya cha biashara. Ukanda Maalumu wa Kiuchumi wa Mkinga unatarajiwa kuleta mabadiliko katika maendeleo ya kiuchumi na ushirikiano barani Afrika kwani mradi huu ni kama lango la zaidi ya nchi 18. Mradi huo wenye thamani ya Dola Milioni 300 sawa na Sh.699 Bilioni, mradi huo utaleta umahiri ya kiuchumi barani Afrika utakaofikia ekari 650 zinazoongoza maendeleo endelevu na kiuchumi barani Afrika. Mradi huo una teknolojia za kiwango cha kimataifa kama Akili Bandia yaani Artficial Intelligence (AI), Biashara ya Mtandaoni (E-commerce) na biashara ya kidijitali na kuifanya kuwa ya kipekee katika eneo hilo.
Mradi huu unalenga kujenga miundombinu muhimu kwa Mkinga ili kuimarisha uchumi na kujenga msingi wa maendeleo kwa kuzingatia mikataba kati ya Mataifa ya Afrika kama vile AfCFTA, EAC, SADC,
AGOA na mikataba mingine mingi," alisema Shady El Zeki, Mjumbe wa Bodi kutoka Zworld.
Wawezeshaji hao wamethibitisha kuwa hadi sasa jumla ya wawekezaji watano kutoka mataifa mbalimbali wameonyesha nia ya kuwekeza fedha, ikiwemo Brazil, Misri, Tunisia, Bulgaria, GCC, Ufilipino na India.
Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 zenye uchumi unaokua kwa kasi barani Afrika. Kwa miaka 10 iliyopita, uchumi wa nchi ulikua kwa wastani wa asilimia 7 (7%). Na Julai 2020, Benki ya Dunia (World’s Bank) iliipandisha rasmi nchi ya Tanzania na kuwa nchi ya kipato cha kati. Mafanikio haya yanaweza kuhusishwa na utulivu wa kisiasa na kiuchumi, sera na viongozi wazuri, pamoja na umoja na amani. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Siginon Logistics E.A Limited, Ali Mohammed, alisema kampuni hiyo imetengeneza mazingira mazuri na rafiki ili kuruhusu uwekezaji kwa kushirikiana na mashirika ya
serikali, hatua ambayo itapunguza michakato isiyo ya lazima. "Katika kipindi cha wiki mbili, mwekezaji mwenye nia ataweza kupata kibali cha kuwekeza katika mradi huu baada ya kuzingatia masharti na vigezo vilivyopo. Tunatarajia kuanza utekelezaji wa awamu ya kwanza, mwanzoni mwa mwaka 2023 na tunawakaribisha wawekezaji wa ndani na nje kutumia fursa hii,’ Alisema. Vilevile, serikali ya Tanzania itanufaika na uwekezaji huu wa kigeni na kuifanya kuwa miongoni wa nchi zenye maendeleo ya kiuchumi kwenye nchi za Afrika. Na mkoa wa Tanga utakuwa na mabadiliko kwa kupata faida ya ajira na ukuaji wa uchumi vilevile kuwa kitovu cha biashara, baharini na usafiri wa anga.
Kuhusu Mradi wa Mkinga (MKINGA ECONOMIC ZONE):
Kutumia akili bandia yaani artificial intelligence (AI), teknolojia ya usambazaji data (Blockchain Technology) na leseni za biashara za kawaida, kuruhusu makampuni kutoka Duniani kote kuungana na
kufanya biashara kutokea Dubai. Aina mpya ya biashara kupitia mtandao (e-commerce) inayojulikana kama smart commerce, ambayo hutumia algorithms, akili bandia (Artificial Intelligence-AI) na mitandao itakayoendesha uvumbuzi ndani ya minyororo ya ugavi (Supply Chain).
Post A Comment: