HALMASHAURI ya wilaya ya Makete mkoani Njombe imepiga marufuku kuchinja Nguruwe na kula nyama (Kitimoto) kwa muda usiojulikana kwasababu ya taarifa za uwepo wa ugonjwa wa homa ya Nguruwe wilayani humo hususani katika kata ya Tandala kutokana na vifo vya Nguruwe 21.
Afisa Mifugo na Uvuvi wa wilaya hiyo bwana Aldo Mwapinga, ametoa amri hiyo kutokana na vifo vya nguruwe 21 wilayani humo.
"Kata ya Tandala kumeripotiwa dalili za ugonjwa wa homa ya Nguruwe kwahiyo tunaendelea na jitihada za kuhakikisha tunashirikiana na watendaji kuanzia ngazi ya kata hadi vitongoji kutoa taarifa juu ya hali inavyoendelea"Amesema Mwapinga
Amesema serikali imepiga marufuku hiyo hususani katika kata ya Tandala huku pia akizuia utoaji wa Nguruwe kutoka kwenye zizi moja kwenda jingine kwa ajili ya kupandisha kwa jike. Pamoja na kutekeleza maagizo hayo pia ameagiza wananchi kuacha kufukua Nguruwe (Mizoga) waliofukiwa baada ya kufa na kuwachinja kisha kwenda kuuza nyama hizo vilabuni nyakati za usiku kutokana na taarifa zilizoripotowa hivi karibuni wilaya ni humo.
Post A Comment: