Na Theophilida Felician Kagera.
Makamu Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Tanzania bara Komredi Abdulrahamani Omar Kinana ameuagiza uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Kagera kuona ni namna gani ya kuziondoa changamoto za vikwazo wanavyokumbana navyo wananchi katika maeneo ya mipakani pale wa napokuwa na uhitaji wa kuvuka kwenda Nchi za Rwanda, Burundi, na Uganda.
Kinana ameyaagiza hayo wakati akiwahutubia wanachama hicho pamoja na wananchi wote kwenye mkutano uliofanyika Manispaa ya Bukoba ambapo amesema kuwa vikwazo kwa wananchi wanapotaka kwenda kwa majirani kwa ajili ya shughuli za kawaida waachiwe tuu.
" Unakuta mtu ana familia yake tena na watoto au labda anakamzigo anaenda kukauza uganda pengine anatokea Muleba, Missenyi Au Bukoba Mjini akifika mpakani tuu utasikia simama hapo! we nani? umebeba nini? Unatoka wapi?unaenda wapi? wakati anaona kabisa naelekea Uganda, la hasha! imekuwa mahakama?"ameuliza Komredi Kinana huku wananchi wakimwitikia kwa makofi mazito.
"Ndugu Mkuu wa Mkoa mna mpaka na Rwanda mna mpaka na Burundi, mna mpaka na Uganda rahisisheni mambo haya fanyeni biashara na watu wa nchi hizi tupunguzeni kashikashi kwa wananchi ili wajishughulishe kwa uhuru hii itasaidia kuinua kipato chao na Mkoa kwa ujumla"Kinana akieendelea kusisitiza.
Katika hatua nyingine amegusia changamoto zinazo husu zao la kahawa kwa ujumla amesema kwa msimu wa mwaka huu Serikali imeanzisha utaratibu mzuri wakulipunguza zigo la kukatwa utitiri wa tozo kwa wakulima katika zao hilo, lengo ni kutaka mkulima naye anufaike na kahawa yake haswa.
Aidha ameongeza kwakutoa wito juu ya watumishi wa ushirika ya kwamba kila mmoja awe anashamba na kama hana shamba aondoke Mara moja au afukuzwe make atakuwa hana sifa tena ya kuwa kiongozi wa ushirika kwani kiongozi wa ushirika bila shamba ni njia za kuuhujumu ushirika na wananchi.
Hata hivyo amewasihi wana CCM kuwa macho na kuwachagua viongozi Bora ndani ya chama kwa ngazi zilizobakia ambazo ni wilaya na mkoa huku akionya kuwa katu wasiwachaguwe watu watakaokiuka misingi na katiba ya chama hicho kwakutumia njia za vitendo vya Rushwa ili wawachuguwe kwani kiongozi wa hivyo hafai kabisa.
Cosintasia Nyamwiza Buhiye ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoa Kagera amemdhibitishia makamu huyo kuwa hali ya kisiasa ndani ya chama ni safi na tulivu hivyo anaimani hata chaguzi zilizobakia zitakamilika salama.
Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe Albert Chalamila naye ameielezea adhima yake kubwa ya kuhakikisha Mkoa wa Kagera unafunguka zaidi kiuchumi ili kuondokana na hali ya umasikini na akusema kwamba awali kabisa zipo zinafanyika juhudi mahususi za kuyaruhusu mabasi yanayotokea mikoni na kulala kahama Mkoani Shinyanga yasilale huko badala yake yaje kulala Bukoba "nawambieni ukweli ndugu zanguni wananchi mabasi yataanza kulala hapa Bukoba na hii itasaidia kutuletea pesa hapa" Albert Chalamila Mkuu wa Mkoa.
Post A Comment: