***********************

Naibu Waziri Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amewataka wafanyabiashara wa Tanzania kuchangamkia fursa ya soko la mazao ya chakula nchini Comoro.

Mhe. Kigahe ameyasema hayo baada ya kikao chake na Balozi wa Comoro nchini Tanzania, Dkt. Ahmada El Badaoui pamoja na wafanyabiashara wa Tanzania na Comoro kilichofanyika mkoani Dodoma.

Aliwataka Watanzania kutumia fursa hiyo kwani nchi ya Comoro wanauhitaji wa chakula hasa mchele na nyama hivyo alitoa rai kwa wazalishaji na wafanyabiashara kuchangamkia fursa ipasavyo.

“Wamekuja kuona namna gani wanaweza kupata bidhaa mbalimbali, hususani mihogo, mchele, nyama, kuku, maziwa na saruji, pamoja na vifaa vya ujenzi.”

Mhe. Kigahe ameitaka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) na Wakala wa Vipimo (WMA) kuratibu vizuri matumizi ya fursa ya soko la Comoro ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa Wazalishaji, Wafanyabiashara na Wakulima wanafaidika na soko hilo.

Awali Mhe. Balozi wa Comoro nchini Tanzania, Mhe Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed, aliwahakikishia wafanyabiashara wa Tanzania uwepo wa soko la uhakika nchini Comoro.

“Tuna mahitaji ya bidhaa za chakula kama vile mihogo, mchele, nyama, maziwa na vifaa vya ujenzi.”Alisisitiza.

Balozi Dkt. Ahamada El Badaoui alianisha changamoto wanayokutana nayo kwa sasa ni bei kubwa ya bidhaa hizo. Hivyo ameiomba Serikali ya Tanzania kuangalia uwezekano bidhaa hizo kupatikana kwa bei nafuu hususan kwa nchi ya Comoro.

Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: