Na; Fredy Mgunda, Iringa.


Kampuni ya SHAFA Agro iliyopo mkoani Iringa katika Kijiji cha kidamali kata ya NZIHI imetoa ajira zaidi ya 131 kwa wananchi wanaolinguka shamba SHAFA lengo likiwa ni kukuza uchumi wa wananchi wa kata hiyo.


Akizungumza na blog hii Afisa uendeshaji shamba la SHAFA Mkadam Mkadam alisema kuwa wameamua kutoa ajira kwa wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya jirani na shamba hilo ili kukuza uchumi kwa wananchi wa kata hiyo,lakini pia wameajili wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi na nje ya nchi.


Alisema kuwa wafanyakazi wote wamefunguliwa akaunti benk na mishahara yao wanachukulia huko,wanawalipia NSSF,WCF na hivi karibuni wanampango wa kuwakatia bima ya afya ya NHIF kwa ajili ya usalama wa afya zao na familia zao na wafanyakazi wote wamepewa mikataba ya kazi ambayo inawalinda wafanyakazi wawapo kazini


Mkadam alisema kuwa kampuni ya SHAFA Agro imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia kukuza uchumi wa wananchi na kupatia maendeleo kwa njia mbalimbali kama vile kuchangia katika shughuli za maendeleo ya Vijiji vyote ambavyo wanaolizunguka shama hilo.


Alisema kuwa wameshachagia zaidi ya madawati 162 kwa shule ya sekondari na msingi ya kidamali,wamechangia kiasi cha shilingi million nne (4,000,000) kwa ajili ya ukarabati wa ofisi ya Kijiji cha kidamali,kulipa mishahara kwa walimu watano kwa miezi nane huku kila mmoja akilipwa kiasi cha shilingi laki moja na nusu (150,000) na pia wamechangia michango mbalimbali kwenye makanisa na misikiti.


Mkadam alisema kuwa wametafuta gari maalumu kwa ajili wananchi kubebea maiti kutoka mjini hadi hapo kijijini kwa kuwa wameona unapotokea msiba wananchi wanakuwa wanahangaika sana kupata usafi hivyo kampuni ikaamua kuwasaidia kwa njia hiyo ili kudumisha mausiano ya mwekezaji na wananchi.

Alisema kuwa wamekuwa wakichangia katika sekta mbalimbali kama vile michezo kwa kuchangia timu ya mpira wa miguu ya kidamali kwa kuwapa pesa na kukarabati uwanja wa mpira wa Kijiji hicho,wamewachangia wanafunzi wawili wa elimu ya juu huku kila mmoja wakimpa kiasi cha shilingi laki tano(500,000).


Mkadam alimazia kwa kusema kuwa wanampango wa kutoa elimu ya ufugaji bora wa ng'ombe kwa wananchi ili hapo baadae waweze kuwapatia ng'ombe waanze kufunga huku wakiwa wanaelimu ya kutosha juu ya ufugaji bora wa ng'ombe wa maziwa.


Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nzihi ambaye ndio mwenyekiti wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Stephen Mhapa alisema kuwa wanapongeza kampuni ya SHAFA Agro kwa uwekezaji ambao wameufanya katika Kijiji cha kidamali kwa kuwa uwekezaji huo unatija kubwa katika kukuza uchumi wa wananchi na kuleta maendeleo kwa wananchi.


Mhapa alisema kuwa wawekezaji hao wameshachagia mambo mengi na wameahidi kuendelea kuchangia maendeleo ya wananchi pale ambapo inahitajika kwa maslai ya mwekezaji na wananchi wa Kijiji cha kidamali na kata ya Nzihi kwa ujumla wake.


Alisema kuwa kitendo cha kuwaajili wananchi wengi kutoka katika Kijiji cha kidamali na kata ya Nzihi kumesaidia kuongeza ajira kwa wananchi na huku wakiendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ufugaji bora wa ng'ombe wa maziwa kumesaidia wananchi kujikwamua kiuchumi



Share To:

JUSLINE

Post A Comment: