



**********************
CHUO cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimeshiriki katika maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani Kilwa mkoani Lindi ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya mwaka 2022 " Teknolojia mpya Kwa uchukuzi wa kulinda mazingira, inaonesha hitaji la kuunga mkono uhifadhi wa mazingira katika shughuli za usafiri na usafirishaji katika bahari, maziwa na mito duniani".
Maadhimisbo haya yatafanyika Kwa muda wa siku nne kuanzia tarehe 26 - 29/09/2022 ambapo shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwa ni pamoja na kutembelea Mialo ili kukutana na watumiaji wa vyombo vidogo vya usafiri na usafirishaji majini kwa lengo la kutoa elimu, kufanya elimu mashuleni na kutoa elimu ya usafiri na usafirishaji majini pamoja na maonesho katika mabanda maalum yaliyoandaliwa Kwa ajili ya kutoa elimu ya usafiri na matumizi sahihi ya Bahari.
Akizungumza katika maadhimisho hayo leo mkoani Lindi, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Atupele Mwakibete amesema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 inatarajia kununua meli nane za uvuvi za kisasa ambazo zitagawiwa Tanzania Bara nne na Zanzibar nne ambazo zitakuwa chachu ya kuinua uchumi wa bluu.
Pia amesema Serikali inatarajia kujenga bandari ya uvuvi ya kisasa katika wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi ambayo itaongeza fursa za kuinua uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja.
Aidha Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe Atupele Mwakibete alitembelea mabanda mbalimbali kujionea shughuli zinazofanywa na wadau wa Bahari 




Post A Comment: