Raisa Said,Lushoto
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Kalisti Lazaro amesema hapa kuwa zaidi ya watoto 63,100 wanatarajiwa kupatia chanjo ya Polio wilaya lushoto katika kipindi cha siku nne..
Akisungumza katika uzinduzi wa chanjo hiyo ya Polio wilayani humo,Mkuu huyo wa wilaya alihimiza wakazi wa wilaya kuhakikisha watoto wote wanaolengwa na chanjo hiyo wanachanjwa ili kujikinga na ugonjwa huo hatari.
“Chanjo hii ni nuhimu sana. Mwaka jana tulifanya chanjo kama hiyo na hivi sasa tunarudia kwa watoto kuanzia mwaka sifuri na chini ya miaka mitano,” alieleza.
Aliwapongeza wazazi wote ambao wameleta watoto ikiwa ni pamoja na wanaume ambao alisema hiyo ni kujitambua kuwa wao ni wazazi na wanajukumu kwa watoto wao.
Aliwataka wakazi wa wilaya ya Lushoto kuacha imani potofu ili kuwaepusha watoto na ugonjwa. “Kam mtu umewahi kuona mtu aliyelemaa kwa polio hutasita kumleta mtoto wako ili asijekuwa mzigo,” alisema.
Akielezea kuhusu zoezi hilo, Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo alisema kuwa
zoezi hilo litaendeshwa nyumba kwa nyumba ili kufikia lengo.
Aliwataka wakazi wa Lushoto kuwatoa watoto wote ili wachanjwe na
kuwaepusha na ulemavu utokanao na Poilio.
Naye Dr Monica Bila, Mtaalamu Mshauri wa Mkoa anayefanya kazi na
kikosi kazi cha shirika CDCna mwakilishi wa mashirika mengine kama
WHO, Unicef KATIKA Mkoa wa Tanga, alisema kuwa zoezi hilo ni raundi ya
tatu ya chanjo hiyo. Aliongeza kuwa ikiwezekana watafanya raundi ya
nne ili kuwakinga watoto wa Tanzania na mlipuko wa ugonjwa huo ambao
umetokea Malawi na Msumbiji.
Alisema kuwa hakuna taarifa ya mlipuko nchini Tanzania lakini
wanafanya utafiti kubaini watoto ambao wana viashiria vya ugonjwa huo
ili kuzuia.
“Tunataka kuhakikisha kuwa watoto wote wa Tanzania wanapata chanjo
hiyo kuwaepusha na ugonjwa huo,” alisema.
Hata hivyo Wananchi wa Wilaya hiyo wamesema kuwa watakuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kupata chanjo hiyo ya polio.
Mwanaisha Shelukindo Alieleza yeye anawatoto watatu lakini wote walikuwa wakipatiwa chanjo ya polio hivo atawahamasisha na ndugu zake wawapeleke watoto wao hasa katika siku hizi nne zilizopangwa kwaajili ya utoaji wa chanjo hiyo.
Post A Comment: