Julìeth Ngarabali. Pwani
Watoto zaidi ya 260,000 mkoani Pwani wanatarajiwa kupewa matone ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio mkoni humo katika awamu ya tatu ya kampeni hiyo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Dokta Gunini Kamba amesema lengo ni kuwafikia watoto wote waliopo Mkoa wa Pwani wenye umri chini ya miaka mitano bila kujali kama walishapata chanjo hiyo kipindi chà nyuma.
Amesema ,katika kufikia malengo hayo Mkoa umeweka mkakati wa kuhakikisha timu ya uchanjaji inapita nyumba kwa nyumba,sokoni,Shule za Chekechea na ,Nyumba za ibada.
"Ni muhimu kila mtoto apate chanjo hii ili kuimarisha kinga yake na kuzuia ugonjwa usiingie nchini ,chanjo ni zawadi ya maisha kwa mtoto ,hivyo sote inatupaswa tuelewe kuwa jamii iliyochanjwa ni jamii yenye afya bora kwa maendeleo ya Taifa,"amesema Dkt.Kamba
Amesema kuwa,Mkoa ulifanya vizuri katika chanjo ya awamu ya pili kwakuwa ulivuka lengo la uchanjaji kwa asilimia 131 ya walengwa wote na kwamba matarajio ni kufanya vizuri zaidi katika awamu hii ya tatu.
"Awamu ya pili ya chanjo hii ya Polio Mkoa wa Pwani tulichanja watoto 263,851 lakini katika awamu hii malengo ni kuchanja watoto 263,990 waliopo katika Mkoa wa Pwani,"amesema Dokta Kamba
Awali Mratibu wa chanjo Mkoani humo Dokta Abbas Hincha, amesema kuwa chanjo hiyo ni salama na haina madhara yoyote.
Baadhi ya wakazi wa Kibaha wameipongeza Serikali kuendelea kulinda afya za watoto nchini .
Utoaji chajo hiyo hapa nchinì ni sehemu pia ya utekelezaji Programu Jumuishi ya Taifa ya malezi . makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ,( PJT _ MMMAM ) 2022/2025 -26 inayolenga kujibu changamoto za mahitaji kwa watoto ili kuwekeza kwenye maendeleo ya ukuaji.
Post A Comment: