MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amesema Chama hakitamvumilia mwanachama yeyote ambaye anataka kuwania nafasi ya uongozi kwa kutumia udini, ukabila na ukanda.
Amesisitiza Chama kinawatafuta watu wa namna hiyo na endapo kitaelezwa kuna mtu anashughulika na ukabila, udini na ukanda jina lake litakuwa la kwanza kuondolewa katika orodha ya wanaowania nafasi za uongozi ndani ya CCM.
Kinana ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM Mkoa wa Kigoma ambapo akiwa katika kikao hicho amepokea taarifa ya uwepo wa baadhi ya wana CCM wanaotumia dini na ukabila hususan katika kipindi hiki cha uchaguzi wa ndani wa Chama kushawishi wapigakura.
“Mtu wa kwanza kupunguzwa ni yule ambaye unaambiwa anahangaika na ukabila huyu kata na mwondoe katika orodha, huyu anashughulika na ukabila tunasema mwondoe kwenye orodha. Huyu ana mhukumu mtu kwa dini tunawaambia muondoe kwenye orodha.
“Jambo moja niliseme ambalo lipo katika taarifa ya Katibu wa CCM wa Mkoa (Mobutu Malima) kwamba unapofika wakati wa uchaguzi, Kamati ya Siasa imeonesha ujasiri wa kuandika kuna tatizo la ukabila, ukanda na udini.
“Ukiona kiongozi anahangaika na ukabila, kwa maoni yangu mimi hufai hata kupigiwa kura kwa sababu kila mtu ana sifa zake, tumpime mtu kwa sifa, si kwa kabila, sijui kama mnakumbuka hotuba ya Baba wa Taifa ya ukabila, kwamba tunakwenda karne ya 21 ukiwa umepanda basi la ukabila.
“Na hili lilimuudhi sana Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, wako wakuu wa Wilaya wametoka mikoa mingine kabisa, wako watu ambao wameishi hapa (Kigoma) na Watanzania wenzao, watu wanawajua, wanawaheshimu, wanawathamini.
“Wanagombea, wana sifa, wanafaa, wana msaada halafu unamhukumu kwa kitu kimoja tu, kabila lake, kweli sawa hii? Ni kiongozi aliyefilisika nataka niwaambie haya mambo sio ya wanachama bali yanatengenezwa na viongozi,” alisema.
Alifafanua kuwa kiongozi anaona mambo yake hayaendi vizuri na fursa ya kuchaguliwa haipo, anahamia kwenye hoja za ubaguzi.
“Wanachama hawana hizo sifa, mtu achaguweli kwa sifa zake, mtu achaguliwe na apimwe kwa uwezo wake.
“Mtu apimwe kwa historia yake ya utendaji lakini usifike mahali ukasema huyu kabila langu, kabila lako hovyo, kabila lako uvivu, kabila hana uwezo, kabila lako hafai, hajui hata anachokiomba.
“Lakini unasema kabila langu, oooh tunatoka eneo moja, haya ukishamchagua mnayetoka eneo moja anakusaidia nini? Hakuna, hana mawazo, hana jambo jipya, hana la kukwambia. Nyie ni mashahidi nchi yetu hii imeongozwa na watu waliotoka kwenye makabila madogo.
“Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kabila lake ukihesabu wako wangapi, sijui hata kama walikuwa wanafika 100,000 lakini aliongoza nchi hii miaka 24, mpaka leo hatujamsahau Mwalimu kwa uongozi bora, hatumhukumu kwa kabila lake , hapana, tuna mhukumu kwa uwezo.
“Hivyo hivyo Mzee Ali Hassan Mwinyi anatoka kwenye eneo dogo, mzee Mkapa ametoka eneo dogo lakini amefanya kazi kubwa nzuri , sasa tukikaa watu tunawahukumu kwa ukabila na ukiona mtu anahangaika na ukabila tafadhali mkateni jina lake, achenani naye,”alisema Kinana.
Alisisitiza kwamba CCM inawatafuta hao watu wa namna hiyo na kwamba wakiambiwa kuna mtu anashughulika na ukabila, udini na ukanda hataachwa na bahati nzuri hiyo habari ikaja kwetu(CCM) , maana yake kazi kubwa waliyonayo mwaka huu ,watu waliojitokez kugombea nafasi za uongozi ni wengi na wenye sifa zote.
“Kwa hiyo hatuna ufuraka wa watu waliogombea , kazi kubwa tulinayo ni kupunguza watu. Mtu wa kwanza kupunguzwa ni yule ambaye unaambiwa anahangaika na ukabila, udini na ukabila.Mtu huyo tunaondoa jina lake kwenye orodha ya wagombea,”alisema Kinana.
Aliongeza Mwalimu Nyerere alikuwa anasema hatutafuti askofu, hatutafuti sheikh wala au Imamu wa Msikiti, bali wanatafuta kiongozi wa kuongoza wanzake.“Sasa ndugu zangu viongozi ninyi ndio mko hapa , Chama hiki Mkoa wa Kigoma ni ninyi.Ninyi ndio mnaotengeneza muelekeo wa Chama chetu, ndio mnaomua nani awe nani,
“Ninyi ndio mnaotengeneza uhai wa hiki Chama, mnaaamua Chama hiki kiwe na uhai au kisiwe, lakini kama uhai wa chama , maendeleo ya mkoa huu msingi wake utakuwa dini ya mtu itakuwa tatizo kubwa sana, niwaombe ndugu zangu msihangaike na hili jambo, angalieni uwezo wa mtu hata kama ni ndugu yako,
“Hata kama ni ndugu mmezaliwa naye na hana uwezo mwambie tu we ni ndugu yangu lakini kwa bahati mbaya uwezo huna .Mtu anakuleta meseji ananiambia Makamu Mwenyekiti naomba nije ni kuone, naamuliza kuna shida gani, ooo nina jambo langu, niambie kwenye simu , aah ni vizuri tukaonana.
“Basi mimi najua hiyo kuonana ina maana yeke , basi namwambia njoo saa fulani kama nyumbani au ofisini akija anakwambia nagombea .Unagombea nafasi gani?Nagombea nafasi fulani , halafu unamuuliza maswali ya msingi, si muulizi kabila, simuulizi dini yake bali namuuliza maswali ya msingi,”alisema Kinana.
Alisema anamuuliza huko kwenye mkoa unaotaka kugombea wewe Wilaya ziko ngapi?Anakwambia anadhani kama.“Sasa kama unaanza na nadhani hata fuhai kugombea na kushauri achana na kuombea.Unamuuliza majimbo ya wabunge yako mangapi, hajui na anataka kugombea.
“Lakini ndio hao wakirudi msingi wa kutafuta uongozi sio uwezo ,sio sifa bali anachoona kwake atarudi na atazungumza na jamaa zake ili wamsadie.Na mimi namwambia mtu ukweli , namuuliza maswali ya msingi, swali la kwanza, la pili la tatu akishindwa nawambia usipoteze muda wako , usijipe presha isiyo na sababu
“Unataka ushauri mzuri kwangu achana na hili jambo si lako huliwezi , sasa ananiambia baada ya hilo unanishauri nini?Namwambia ndio nimeshakushauri achana nalo.Hakuna ushauri mwingine zaidi ya hapo , kwa hiyo wako watu wengi sana wana uwezo , wanafaa na wengine wana uwezo mzuri , mabingwa, watu waadilifu, mahodari , lakini kila akitazama maneno yanayosemwa na udini udini, ukabila anaamua kulaa mbali.
“Hapa hapanifai , nikitaka kugombea nitaambiwa mimi sio kabila lako, kwa hiyo tunawakosa watu wazuri kwasababu ameona wale wapiga kura wameweka vigezo vya hovyo na wapiga kura wameweka vigezo vya hovyo kwasababu wanaowangoza ndio wamewakea hivyo vigezo , ndugu zangu hii nchi imeongozwa vizuri na viongozi.
“Baba wa taifa mwalimu Nyerere, aliwahi kusema karne hii ya 21 si karne ya udini , nadhani si karne ya ukabila , wala ukanda , wala eneo .Mimi nawajua wanachama wengi watanzania wala hili jambo halimo kichwani mwao , wanaopandikiza kwenye vichwa vyao ni mgombea, anataka kugombea unaona kura hazitoshi anaenda kwenye ukabila.
“Na watu wanakwenda kwenye ukabila ni pale anapoona kabila lake wapiga kura wake ni wengi ,anahamia pale kwenye ukabila, kwa hiyo badala ya kutafuta hisia au uwezo wa mtu anatafuta mioyo ya watu kuonewa huruma , kwa hiyo nataka niwasihi ninyi ndio viongozi tunawategemea , Makao Makuu ya Chama pale hatujui watu, ninyi ndio mnaowafahamu watu wote.
“Na ni vizuri ukiona mtu anaendesha jambo kama hilo usimseme pembeni , unamuita, kamati ya siasa ya mkoa inakaa inamuita .Leo nimeletewa meseji kuna mtu mmoja wa halmashauri fulani analeta vurugu msipate naye tabu.
“Mnauliza anafanya nini , anasema yeye kuna watu hataki mtu fulani achukue uongozi , sasa wewe Mwenyekiti si una kura moja kwanini unawanyima wenzako nafasi, anatumia ule uenyekiti wa halmashauri , nikawaambia jambo lake rahisi mleteni kwenye Kamati ya maadili , tumjadili, tutamshughulikia, basi.
“Hakuna namna nyingine, na Chama hiki kina kanuni, Katiba, kina maadili , kanuni za uongozi na kanuni za utumishi, zote zimeandikwa na kila kitu kimeandikwa vizuri wala hatutoi nje ya utaratibu , na kwenye maadili adhabu imeandikwa humo ndani, kila kitu kipo hatuzui mambo.”
Post A Comment: