Raisa Said,Tanga


Benki ya Dunia imetoa msaada wa sh  17 Bilioni  kwa serikali ya Tanzania Kwa lengo  ya kuimarisha huduma ya mama na mtoto Ikiwemo kupunguza vifoa vitokanavyo na uzazi.


Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu hivi karibuni wakati  alipokutana na wadau kutoka shirika la GFF (global Financing Facility kutoka Benki ya Dunia ambao wanafadhili mradi wa kitita cha uzazi Salama katika hospitali ya rufaa ya Bombo.


Amesema kuwa fedha hizo zinatarajiwa kutumika katika ununuzi wa vifaa tiba na  kuwajengea uwezo watumishi wa afya ili kubaini changamoto za mama mjamzito katika hatua ya awali na hivyo kuweza kudhibiti madhara .


"Wadau wa GFF wamefadhili huduma ya mama na mtoto katika mikoa mitano hapa Nchini na tayari matokea ya awali yameonyesha kupungua Kwa vifo Kwa zaidi ya asilimia 50"amesema Ummi Mwalimu.


Nae Meneja Mradi wa kitita cha uzazi salama Dk Pascal Mdoe amesema kuwa mradi huo unatekelezwa katika mikoa ya Manyara,Tabora,Shinyanga,Geita na Mwanza .


"Mradi umeweza kufika katika hospitali 30 katika awamu ya kwanza lakini awamu ya pili tunatarajia kufikia hospitali 100 lengo ni kuhakikisha tunamalizia changamoto ya vifo vya uzazi na watoto wachanga"amesema dk Mdoe


Hat hivyo Serikali ya Tanzania kupitia sera ya afya 2007 imewekeza sana katikakuboresha uhai wa mtoto kupitia utoaji wa huduma bure za afya Kwa kina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.


Mpango mkakati wa Taifa was kuboresha afya ya uzazi ,mzazi,mtoto na vijana nchini Tanzania (2016 - 2020) umeweka  mazingira wezeshi ya kupunguza  magonjwa ,vifo vya akinamama,watoto wachanga ,watoto na vijana  Kwa kutoa  huduma  bora ,endelevu na jumuishi  zinazowafikia watu wote katika  ngazi mbalimbali za utoaji huduma  bora  katika vituo Cha afya  na kwenye jamii.


Hivyo basi matokeo  ya afya  za wanawake  na watoto yameendelea  kuwa bora .Taarifa  za tafiti TDHS-MIS  za 2015- 16  zinaonyesha mafanikio  makubwa  ya  asilimia 98.9 ya mahudhurio  ya mama wajawazito  waliohudimiwa na wataalam mwenye  ujuzi kutoka asilimia 96 mnamo mwaka 2010.

Share To:

Post A Comment: