Mkuu wa wilaya Serengeti Dkt.vincent Mashinji amewataka wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri ya wilaya ya Serengeti kwa ajili ya kuwawezesha kujikuza kiuchumi kuhakikisha wanairejesha mikopo hiyo kwa wakati ili iweze kuwasaidia wananchi wengine lakini pia kujiongezea kiwango cha ukopeshwaji,ambapo katika robo hii wilaya imetoa kiasi cha Tsh.152,4600,000/=
Akizungumza na Wanufaika wa mikopo hiyo ambao ni wanawake,vijana na walemavu baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa utoaji wa mikopo kutoka idara ya maendeleo ya jamii amewasisitiza makundi yote kurejsha mikopo hiyo kwa wakati.
‘’Unapopewa mkopo lazima urejeshe,lakini sasa kumekuwa na tatizo kwenye halmashauri yetu watu wanapewa mikopo na wengine hawarejeshi tatizo hili ni kubwa kwa vijana’’alisema Dkt.MashinjiKatika hatua nyingine amewapongeza wanawake kwa kuwa mstari wa mbele kwa kurejesha mikopo ya kwa wakati na kuwataka makundi mengine inayonufaika na mikopo hiyo kurejesha mikopo hiyo kwa wakati,kwa uwa imekuwa ni sehemu ya ajira na hivyo kupunguza uhalifu.
Aidha amempongeza Mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya Serengeti Mhe.Ayub Makuruma kwa usimamizi mzuri wa mikopo hiyo ya asilimia 10 na utaratibu mzuri wa utolewaji wa mikopo hiyo.
Nae,Mbunge wa jimbo la Serengeti Dkt.Amsabi mrimi Amempongeza Mhe rais samia Suluhu hassani kwa kazi kubwa anayoifanya kwa ajili ya kuleta maendeleo kwenye jamii,lakini pia amevipongeza vikundi vyote ambavyo vinarejesha mikopo hii kwa wakati ,amewataka wanavikundi hao kujikita Zaidi kwenye kufanya kazi na kujitoa Zaidi kwenye shughuli za maendeleo kutoka na mikopo hii.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti ambae pia ni diwani wa kata ya busawe Mhe.Ayub Makuruma amewataka wanufaika wa mikopo hii isiyo riba kuitumia vizuri ili kuinua maisha yao ‘’watu wamekuwa wakiogopa kuichukua mikopo hii ,mikopo ndiyo salama na ya uhakika ‘’alisema Mhe makuruma
Aliongezea kwa kusema kuwa mikopo hiyo ni kimbilio sahihi na hakuna haja ya kuhofu amewahakikishia wanavikundi kuwa pesa za mikopo zipo hivyo vikundi viendele kujitokeza ili kupata mikopo hiyo na kutumia kujikuza kuichumi na sio kuitumia kwa njia tofauti.Kabla ya Kupatiwa mikopo hiyo wanufaika kutoka kwenye vikundi mbalimbali walipatiwa mafunzo ili waweze kuitumia mikopo hiyo ikawe na tija
Post A Comment: