Na John Walter-Manyara
Imeelezwa kuwa Mabasi yanayofanya safari mikoani yataanza kukata tiketi kwa mfumo wa mtandao kuanzia Septemba Mosi mwaka huu.
Akizungumza mjini Babati wakati wa ukaguzi wa magari yanayobeba wanafunzi, Meneja mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) katika mkoa wa Manyara Joseph Michael amesema kuanzia siku ya Alhamisi septemba mosi abiria wotewatakata tiketi za kusafiria kwa njia ya mtandao (TIKETI MTANDAO).
Afisa huyo ameeleza kuwa kuanzia siku hiyo basi ambalo litakuwa halitoi tiketi ya kielektroniki halitaruhusiwa kuondoka na faini yake ni shilingi laki mbili na nusu (250,000) papo hapo.
Abiria wametakiwa kuacha kutumia tiketi zilizoandikwa kwa mkono na badala yake kutumia zinazotolewa kwenye mashine (POS) kununua wenyewe kupitia simu zao au Computer.
Mfumo wa tiketi za kielektroniki ukianza kutumika rasmi kwa mabasi yote nchini kupitia mfumo huo, abiria ataweza kukata tiketi na kuilipia moja kwa moja kwa njia ya mtandao bila kupitia kwa mawakala wa mabasi kama ilivyozoeleka.
Post A Comment: