MKURUGENZI wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akisani mkataba na Kiongozi wa Mradi wa EACOP Jerome Betat wakati makubaliano na Kampuni ya kusimamia Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi ya utekelezaji wa miradi miwili ya maji unaokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Bilioni 3 kulia anayshuhudia ni MBunge wa Jimbo la Tanga na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Fungo Ally na katikati aliyevaa shati la drafti ni Mstahiki Meya wa Jiji la TangaMKURUGENZI wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akisani mkataba na Kiongozi wa Mradi wa EACOP Jerome Betat wakati makubaliano na Kampuni ya kusimamia Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi ya utekelezaji wa miradi miwili ya maji unaokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Bilioni 3 kulia anayshuhudia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Fungo Ally na katikati aliyevaa shati la drafti ni Mstahiki Meya wa Jiji la TangaMKURUGENZI wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akisani mkataba na Kiongozi wa Mradi wa EACOP Jerome Betat wakati makubaliano na Kampuni ya kusimamia Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi ya utekelezaji wa miradi miwili ya maji unaokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Bilioni 3 kulia anayshuhudia ni MBunge wa Jimbo la Tanga na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Fungo Ally na katikati aliyevaa shati la drafti ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga
Na Oscar Assenga, TANGA
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) leo imeingia makubaliano na Kampuni ya kusimamia Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi ya utekelezaji wa miradi miwili ya maji unaokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Bilioni 3.
Mradi huo utasaidia wakazi watakaopitiwa na boma hilo na maeneo ya jirani wapatao 26,563 ambapo utawezesha pia kambi ya kampuni ya kusimamia Bomba la Mafuta ghafi kutoka Uganda (EACOP) kupata huduma ya maji kwa zaidi ya lita 200,000 kwa siku.
Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa hafla ya utiliaji wa saini makubaliano ya utekelezaji wa mradi huo.
Mhandisi Hilly alisema mradi huo wa maji umezingatia pia ongezeko la Watu,Taasisi na hata viwanda kwa maeneo ya kata za Mabokweni,Mzizima na Chongoleani kufuatia uwepo wa mradi wa Bomba la Mafuta.
Alisema mamlaka hiyo itatumia uwezo mkubwa iliyonao wa usimamizi wa miradi ya maji kuhakikisha kuwa miradi hiyo inajengwa kwa ubora unaostahili na kwa muda mfupi zaidi ya ulioainishwa kwenye mkataba (Miezi 6 kwa Jiji la Tanga na miezi 3 kwa mji wa Muheza).
“Tutatumia njia sahihi na bora katika kuwapata wakandarasi wa miradi wenye uwezo mzuri, waadilifu na wasio na ubabaishaji kuwezesha miradi kukamilika kwa ubora na kwa wakati”Alisema Mhandisi Hilly.
Aidha alisema mradi wa kwanza ni ulazaji wa bomba la maji (DN 200) kutoka Kitisa hadi katika Tangi la Maji lililopo katika nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mjini Muheza kwa umbali wa mita 6000.
Alisema mradi huo wenye thamani ya Milioni 454,836,670 utawezesha Tanga Uwasa kuongeza uzalishaji maji kutoka uwezo wa lita 1,500,000 kwa siku hadi lita 2,000,000 kwa siku toka kituo cha Kilapula.
“Kwa uzalishaji huo wa maji utawezesha Kampuni ya EACOP kambi ya Kitisa kupata maji ya ujazo wa lita 200,000 kwa siku na wananchi wa Muheza Lita 1,800,000 kwa siku huku Tanga Uwasa ikitarajia kuunganisha matawi mapya 1,000 kupitia bomba hilo ambalo litatoa huduma kwa wakazi wapatao 6,000.
Mkurugenzi huyo alisema pia kutakuwa na mradi wa ulazaji wa Bomba la maaji (DN 300) kutoka kona Z Kata ya Kiomoni hadi Chongoleani umbali wa kilomita 22.32 njiani kutajengwa matawi na kuunganisha maji kwa maeneo yote yatakayopitiwa na bomba kuu yaani mitaa ya Mikocheni,Mabokweni, Putini,Ndaoya,Mikweni,Mwanyumbwi,Mpirani na Chongolean.i
Hafla ya utiaji wa makubaliano hayo ulifanyika leo kwenye ofisi za Tanga Uwasa na kushuhudiwa na Mbunge wa Jimbo la Tanga na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakiwemo viongozi mbalimbali na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza.
Akizungumza mara baada ya kumalizika zoezi la utiaji wa saini wa utekelezaji wa mradi hiyo miwili Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hillly alisema kwamba Serikali ilipokubaliana na Serikali ya Uganda kutekeleza mradi wa wa ulazaji wa bomba la mafuta ghafi kutoka hoima nchini Uganda hadhi Chongoleani Jijini Tanga nchini Tanzania.
Alisema mradi huo umefungua fursa nyengine kwa uchumi lakini hapa nchini imeongeza uhitaji wa maji kwa wakazi wa maeneo yatakayopitiwa na mradi wa Bomba la Mafuta na hivyo kuweza kuondokana na changamoto ya huduma hiyo muhimu.
Aidha alisema kwamba Kampuni hiyo inayosimamia mradi huo ya (EACOP) wanahitaji huduma ya maji ambapo kwa eneo la Tanga huduma hiyo inahitajika katika kambi za Chongoleani Jijini Tanga na kitisa iliyopo wilayani Muheza na kila kambi inahitaji lita 200,000 kwa siku na huduma hiyo inatolewa na Tanga Uwasa.
“Tunamshukuru Waziri Jumaa Aweso, Waziri Ummy Mwalimu na Mbunge wa Muheza Hamisi Mwinjuma kwa kuwapigania wana Tanga na wana Muheza kwa jitihada zetu za kufuatilia kwa karibu zimepelekea leo Tanga Uwasa tunatia saini mikataba wa ujenzi wa mradi ya maji katika maeneo ya chongoleani na kitisa na kampuni inayosimamia ujenzi wa bomba la mafuta Ghafi (EACOP) “Alisema
Awali akizungumza wakati wa kutiliana makubaliano hayo,Mbunge wa Jimbo la Tanga na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alisema watu hao wamefanya ustaarabu ya kuwekeza kwenye miradi ya maji ambao utakuwa na tija kubwa kwa wananchi na wao.
Alisema kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na wananchi wa Tanga wanawashukuru kwa kukubaliana na ombi la kusaidia kuongeza upatikana wa mradi wa maji katika eneo la Chongoleani na Muheza.
Alisema wanamshukuru Rais Samia Suluhu kwa sababu amewawezesha wamekuwa na Waziri Aweso mchapakazi anafanya kazi nzuri sana na wamepata Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa wanafanya kazi nzuri sana sasa wamepata hao wawekezaji kuwapa hiyo fedha sasa maji katika kata ya Chongoleani,Mabokweni na Mzizima wakimaliza mradi huo yatatoka siku saba masaa 24 kwa siku.
Alisema wamepata hayo ndio maendeleo ambayo wanayoyasema chini ya Rais Samia Suluhu lakini akiwa kama Waziri wa Afya hayo maji yataondoka kero na kupunguza magonjwa ya kuhara kipindupindu, kichocho kwa sababu watu wanatumia maji ambayo sio safi na salama lakini ni sehemu ya kuwapunguzia mzigo wa kusaka huduma ya maji na hivyo kupata maji kwa wakati na kufanya shughuli nyengine za kiuchumi na kuwalea watoto.
“Kwa niaba ya watu wa Tanga tunawashukuru sana EACOP lakini pia nimeona milioni 450 ambayo inapelekwa Muheza kwa hiyo Muheza inakwenda kuondokana na tatizo la maji kwa kweli nishahukuru sana kwa msaada huu mkubwa wa kutusaidia kwenye suala la maji”Alisema
Alisema anashukuru kwa uamuzi huo na kupongeza jitihada za Tanga Uwasa kwa sababu ilani inasema 2025 upatikana maji mijini uwe asilimia 95 na Tanga sasa wapo asilimia 96 maana yake wameshapita huku na Mkurugenzi alimueleza kwamba wanaweza kupita.
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza Erasto Mhina aliwashukuru Tanga Uwasa kwa niaba ya wananchi wa Kata ya Genge kewa kuwapatia wananchi wake maji safi na salama kwa muda mfupi ujao.
Alisema watu wana kero ya maji katika mazingira ya karibu na Tanga mjini kipekee niwapongeza Tanga Uwasa kwa kuona umuhimu wasiwapatie watu wa Tanga mjini pekee, mradi huo unagharimu karibu milioni 454,836,670 na utakwenda kuwanufaisha wananchi wasiopungua 6000 sio jambo dogo wanawashukuru na watawapa ushirikiano mkubwa unaotakiwa wakati wote.
Hata hivyo Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shilloo amesema shukurani kubwa ziende kwa Rais Samia Suluhu kupitia utendaji wa mawaziri wake Ummy Mwalimu wa Afya,Jumaa Aweso na Maji akiwemo Mbunge wa Jimbo la Muheza Hamisi Mwinjuma kwa kuwasaidiana na uongozi wa Tanga Uwasa kuhakikisha changamoto za maji Muheza na Tanga zinapatiwa ufumbuzi.
Mwisho.
Post A Comment: