Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati utakaosaidia kuharakisha mchakato wa zoezi la sensa ya watu na makazi 


Dc Muro amesema hayo wakati akitatua changamoto ya baadhi ya wananchi wanaoishi mpakani mwa ikungi na singida manispaa katika kijiji cha Chungu ambapo zaidi ya kaya 10 zilikubali kuhesabiwa baada ya kuelezwa kwa mujibu wa ramana na taarifa zilizomo kwenye vishikwambi makazi yao yako chungu na sio kijiji cha mtamaa 


Dc Muro pia amewaomba wazazi ambao ni wakuu wa kaya wanaojishughulisha na kazi za kilimo, ufugaji au ajira ambao wanalazimika kuondoka majumbani asubuhi kuteua wakuu wa kaya wasaidizi na kuwaachia taarifa muhimu zitakazosaidia kujaza haraka dodoso la sensa ya watu na kazi ili zoezi liende kwa haraka


Katika hatua nyingine Dc Muro amesema tayari wamefanikiwa kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili makarani katika siku ya kwanza na ya pili ikiwemo suala la vishikwambi kuishiwa chaji mapema na fedha za wenyeviti wa vitongoji wanaoshirikiana na makarani katika kuzungukia kaya na fedha tayari zimeshalipwa tangu jana kiasi cha elfu hamsini kwa kila kitongoji mwanzo wa zoezi na mwisho wa zoezi watalipwa tena elfu hamsini kukamilisha malipo ya laki moja kila mwenyekiti wa kitongoji ambae atakuwa na karani kwenye zoezi



Share To:

Post A Comment: