Na John Walter-Babati
Mkuu wa wilaya ya Babati ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Sensa wilaya ya Babati Lazaro Twange, amewataka wananchi ambao bado hawajahesabiwa kuhakikisha wanafika katika ofisi za mitaa au kijiji ili kuhesabiwa pamoja na kutoa ushirikiano kwa makarani kwenye zoezi la sensa ya majengo ambalo linaendelea.
Twange amesema hayo mjini Babati wakati akitoa tathmini ya Sensa ya Watu na Makazi katika wilaya hiyo.
Pamoja na mambo mengine,amesema zoezi la Sensa ya watu na makazi mwaka 2022 wilayani Babati kuanzia Agosti 23 hadi 29 lilienda vizuri bila shida yoyote huku vitendea kazi vyote vikiwa salama na bado linaendelea.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya ametoa namba za waratibu wa zoezi hilo mwaka huu ili ambao hawajahesabiwa waweze kuhesabiwa kwa kupiga namba hizo au kutuma ujumbe mfupi wa maandishi na kueleza wapi anapatikana ili makarani wamfikie alipo.
Namba hizo za Waratibu,kwa Babati mjini ni 0784 768 008 na Babati Vijijini ni 0688 105 591.
Post A Comment: