. Muonekano wa mradi wa Tenki kubwa lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita laki moja (100,000) lililojengwa na Kampuni ya Chakwale kwa ufadhili wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani- ni moja ya miradi iliyokamilika na inatarajiwa kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru wilayani humo kesho kutwa Agosti 13 mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo baada ya kukagua mradi wa maji uliojengwa na Kampuni ya Chakwale kwa ufadhili wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani ambao utazinduliwa na Mwenge wa Uhuru wilayani humo keshokutwa.
Na Godwin Myovela, Ikungi.
AGOSTI 13 mwaka huu, ujumbe wa mbio za Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuzindua
miradimikubwa ya kiustawi na maendeleo, ikiwemo mradi wa maji kwa wakazi wa
vijiji vya Ikungi naUnyahati, daraja la Barabara ya Makiungu-Utaho, nyumba za
watumishi na ujenzi wa vyumba vya madarasa ndani ya Wilaya ya Ikungi mkoani
hapa.
Ikumbukwe, kasi ya ujenzi wa miradi itakayozinduliwa na Mwenge wa Uhuru
ndani ya wilayaya Ikungi ni mwendelezo wa miradi mingine mikubwa inayoendelea
kutekelezwa, ikiwemo ujenzi wa chuo kikubwa cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),
ujenzi wa Hospitali ya Wilaya,miundombinu ya barabara na vituo vya kutolea
huduma za afya-ambayo baadhi yakeilitembelewa na kuwekewa mawe ya msingi na
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa-hivi karibuni.
Akizungumza wakati akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa kijiji
cha Ikungi naUnyahati (moja ya mradi unaotarajia kuzinduliwa na Mwenge), Mkuu
wa Wilaya hiyo Jerry Muro alisema kasi kubwa ya ujenzi wa miradi unaoendelea
kwasasa inachagizwa na dhamira safi na upendo wa hali ya juu wa Rais Samia
Suluhu Hasssan kwa wana-Ikungi na wakazi wote wa mkoa wa Singida.
“Natoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais…na niwaombe wakazi wa Ikungi
tuzidi kumtiamoyo kwa kumpa ushirikiano katika kipindi hiki ambacho anapambana
sana kustawisha uchumi na kuleta matokeo chanya ya hali bora za kihuduma kwenye
nyanja zote za kijamii, ikiwemo afya, elimu, maji, na maboresho ya miundombinu
ya Barabara kwa wana-Ikungi na taifa kwa jumla.
Aidha, katika kufanikisha azma chanya ya ujio wa Mwenge wa Uhuru, Muro aliwasihi
wakaziwote wilayani hapa kujitokeza kwa wingi kuupokea, ambapo pamoja na mambo
mengine pia unatarajia kufanya shughuli nyingine-zikiwemo kuzindua Kikosi
Maalumu cha Kupambana na Rushwa, kushiriki kushiriki zoezi la upandaji miti,
kutembelea na kupokea taarifa ya hali halisi ya ugonjwa wa Maralia kutoka
kwenye banda la utoaji elimu lililopo eneo la Puma.
Mabanda menngine yatakayotembelewa eneo hilo ni pamoja na banda la elimu ya
UKIMWI/Vvu, dawa za kulevya, lishe, dawati la malalamiko, sensa ya watu na
makazi na mradiwa vijana (Tehama) kabla ya kuelekea eneo la Issuna Madukani kwa
ajili ya mkesha.
Imeelezwa, kulingana na ratiba baada ya mwenge kupokelewa alfajiri eneo la Njiapanda wilayani hapa utapita kwenye maeneo kadhaa kulingana shughuli zilizoorodheshwa kiitifaki,ikiwemo maeneo ya Shule za Sekondari Siuyu na Issuna, Minyinga, Puma, Ikungi na kishaviwanja vya Issuna Madukani kwa ajili ya risala ya utii na ujumbe mahsusi wa Mwenge, kabla ya kuelekea Kijiji cha Gurungu (Itigi) mapema Agosti 14 kwa makabidhiano.
Post A Comment: