Choroko ni zao la chakula na biashara lenye kiasi kikubwa cha protini na madini ya phosphorus na calicium. Zao hili likilimwa vizuri hutoa mavuno kati ya Kg 400 hadi 900 kwa ekari moja. Hivyo kwa yeyote yule mwenye nia ya dhati ni vyema akajikita katika kuhakikisha analima kilimo hiki.

UDONGO NA HALI YA HEWA IFAAYO.
Choroko hustawi katika udongo wa aina tofauti tofauti usiotuamisha maji.Hulimwa kutoka mita 0 hadi 1500 kutoka usawa wa bahari japokuwa kuna mbegu nyingine zinaweza kukubali zaidi ya ukanda huu.Hili ni zao linalostahimili ukame.


AINA ZA CHOROKO
Kuna aina kuu mbili za choroko ambazo pia zimegawanyika katika makundi mawili,choroko nyeusi na choroko za kijani.



1. CHOROKO ZINAZOTAMBAA-hizi ni choroko ambazo zinarefuka sana na hutambaa sehemu mbalimbali.



2. CHOROKO ZINAZOSIMAA-Hizi ni choroko ambazo zinakuwa kwa kusima kwenda juu.Hizi huchukua muda mfupi kukomaa wastani wa siku 60-70.



KIPINDI KIZURI CHA UPANDAJI WA CHOROKO
Choroko hazihitaji maji mengi hivyo ni budi zipandwe mwishoni mwa msimu wa mvua,Pia zinaweza kupandwa katika shamba lililolimwa mpunga.



NAFASI ZA UPANDAJI WA CHOROKO NA KIASI CHA MBEGU
Choroko huitaji mbegu kiasi cha kilogram 8 hadi kumi kwa ekari moja.
Panda choroko zako kwa nafasi ya sentimeta 30 mastari na mstari na sentimeta 10 shina hadi shina (30 x10 )sentimeta au (40 x 8 )sentimeta.



SAMADI NA MBOLEA ZA VIWANDANI
Kama shmba lako halina rutuba ya kutosha unaweza kuongeza samadi kiasi cha tani tano kwa ekari na pia unaweza kupanda kwa kutumia mbolea ya NPK kg 50 kwa ekari.weka mbolea zote kabla ya kupanda.
Share To:

Post A Comment: