Na,Jusline Marco:Arusha
Halmashauri ya Arusha imewapongeza wadau wa kimaendeleo na asasi binafsi 11 kwa kutambua michango yao katika kufanikisha zoezi zima la mbio za mwenye wa Uhuru kwenye ukarabati wa miundombinu mbalimbali.
Akitoa pongezi hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Suleman Msumi amesema juhudi hizo niza kipekee kwa wadau hao hivyo kama halmashauri wametambua mchangao wao na kuwapatia vyeti vya shikurani kwa mchango wao.
Kwa upande wake mmoja wa wadau hao Dkt.Philemon Mollel(Monaban)ameishukuru halmashauri hiyo kwa kutambua umuhimu wa wadau wa maendeleo na kutoa shukurani hizo za pekee ambazo kwa namna moja au nyingine zimegusa mioyo yao.
"Nishukuru sana baraza la madiwani la halmashauri ya Arusha kwanza kwa kutambua na kukumbuka fadhila za mtu."Dkt.Phillemon Mollel (Monaban)mdau wa maendeleo
Aidha amewataka wadau wengine wa maendeleo na halmashauri nyingine kuiga mfano ambao halmashauri ya Arusha imeufanya wa kukumbuka fadhila za wadau wanaojitoa kwa ajili ya jamii kwasababu jambo kama hilo linagusa mioyo ya watu.
Post A Comment: