Na,
Moses Mashala:Arusha


Bilionea mpya wa madini ya Tanzanite nchini,Anselim Kawishe amefunguka na kueleza kwamba haamini katika masuala ya ushirikina zaidi ya kumtegemea Mungu katika biashara zake huku akisisitiza amepambana miaka yote akimtegemea Mungu.


Pia amebainisha ya kwamba ametumia zaidi ya jumla ya zaidi ya kiasi cha sh 1 bilioni kuhudumia mgodi kwa muda wa miaka takribani 15 kabla ya kupata madinit ghali ya Tanzanite hivi karibuni.


Bilionea Kawishe ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na waandishi wa habari jijini Arusha ambapo alieleza kuwa kwa kipindi chote akifanya biashara zake haamini katika ushirikina zaidi ya kumtegemea Mungu.



“Sitaki kuingia katika ushirikina maana sitaki kumkosea Mungu wangu ninaamini ya kwamba nitakachokipata kutoka kwa Mungu ndicho chenye baraka na kitadumu “alisema Kawishe 


Bilionea Kawishe alisema kuwa hataki mali ya ushirikina na kwamba anamshukuru Mungu kwa kumbariki kupata madini hayo kwa kuwa yana thamani.


Hatahivyo,alifunguka kwamba ametumia zaidi ya kiasi cha sh 1 bilioni kuhudumia mgodi wake kwa takribani miaka 15 kabla ya kufanikiwa t madini ya Tanzanite.


“Nimetumia zaidi ya bilioni moja kuhudumia huu mgodi na kuna wafanyakazi kama 100 hivi wanahitaji kula na matumizi mengine “alisema Kawishe 


Katika hatua nyingine Bilionea Kawishe alifunguka na kueleza kwamba pamoja na kupata fedha nyingi kupitia madini aliyoyapata lakini huenda akapunguza idadi ya marafiki na kuwa karibu na Mungu.


“Pamoja na kupata fedha hizi huenda nikapunguza marafiki nikawa karibu na Mungu na sitabadilika tena “alisisitiza Kawishe 


Bilionea Kawishe alisema kuwa mbali na kujishughulisha na biashara ya madini ya Tanzanite pia amekuwa akijihusisha na kilimo cha mahindi,maharage na alizeti wilayani Kiteto mkoani Manyara.


Naye mkurugenzi mwenza katika mgodi huo,Gasper Hangaya   yeye ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kuyaona madini hayo na kueleza kabla ya kuyaona alishtuka.


Hangaya ambaye kitaalamu ni mhasibu ameeleza kuwa eneo wanalochimba madini hayo awali lilionekana kama ni eneo lisilokuwa na kitu lakini mtaalamu wa maimba aliwatia moyo kwa kuwaeleza kuwa kuna madini eneo hilo.


“Eneo ni kama mita 350 kwenda chini korongoni siku hiyo nilikuwa mwenyewe na mimi ndiye niliyeyatoa hayo madini nilivyoyaona ghafla nilishtuka sana na kisha kufurahi “alieleza Hangaya 



Hatahivyo,amesisitiza kuwa endapo akipata nafasi ya kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan atamweleza kuwa serikali iongeze idadi ya wataalamu wa sekta ya madini hususani kutoka vyuoni kwa kuwa bado kuna uhaba mkubwa upande wa wataalamu .


Mwisho

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: