Wizara ya Fedha na Mipango ni moja ya washiriki katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam maarufu kama Maonesho ya Sabasaba.

Katika maonesho hayo Wizara, imeshiriki pamoja na baadhi ya Taasisi zake zikiwemo Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Kampuni ya Uwekezaji ya UTT- AMIS, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA), Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), Tanzania Commercial Bank( TCB), Hazina Saccos, Mfuko wa Self, Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA), Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma (PPAA), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA).
Wizara na Taasisi zake inashiriki katika maonesho haya kwa lengo la kutoa elimu kwa umma. Maonesho haya ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yalianza rasmi tarehe 28 Juni 2022, yanatarajiwa kufungwa 13 Julai, 2022.
#sabasaba2022
Share To:

Post A Comment: