Dodoma, Jumatatu, Julai 18, 2022. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kwa makala ya tatu ya mbio za NBC Dodoma Marathon zinazotarajiwa kufanyika Jumapili tarehe 31 Julai 2022.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Dodoma kuhusu hali ya maandalizi ya mbio za Marathon, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka alisema kuwa jiji hilo lina uwezo wa kutosha kuwapokea na kuwakarimu zaidi ya wageni 7,000 watakaofika mjini hapo kushiriki mbio hizo. “Nataka nimhakikishie kila mtu kuwa Dodoma iko tayari kuwapokea wakimbiaji wote na kukidhi matarajio yao. Tuna malazi, chakula na miundombinu ya kutosha kuhudumia wageni wote, wasiwe na wasiwasi wowote” alisema.
Mtaka pia alitangaza kuwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa amekubali mwaliko wa kuwa Mgeni Rasmi wa mbio hizo zinazolenga kukusanya fedha za kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake nchini.
Mheshimiwa Mtaka pia aliwataka wananchi wa Dodoma kuzipokea mbio hizo kama dirisha la kiuchumi na kujiandaa kuendena na ongezeko la mahitaji ya kijamii. “NBC Dodoma Marathon italeta karibu watu 7,000 mjini; watahitaji chakula, malazi, mavazi, usafiri, na aina nyinginezo za burudani. Shime tuitumie fursa hii kujipanga vilivyo. Dodoma ina mengi ya kutoa; tuchangamkie fursa hiyo”. Alisema.Mtaka pia alitangaza kuwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa amekubali mwaliko wa kuwa Mgeni Rasmi wa mbio hizo zinazolenga kukusanya fedha za kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake nchini.
Mheshimiwa Mtaka pia aliwataka wananchi wa Dodoma kuzipokea mbio hizo kama dirisha la kiuchumi na kujiandaa kuendena na ongezeko la mahitaji ya kijamii. “NBC Dodoma Marathon italeta karibu watu 7,000 mjini; watahitaji chakula, malazi, mavazi, usafiri, na aina nyinginezo za burudani. Shime tuitumie fursa hii kujipanga vilivyo. Dodoma ina mengi ya kutoa; tuchangamkie fursa hiyo”. Alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi alisema Benki hiyo inafuraha kuandaa tena mbio zake jijini Dodoma baada ya mafanikio awali. “Dhamira yetu ni kusaidia kuchangisha zaidi ya shilingi milioni 200 na kuzipeleka katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake nchini. Saratani ya Shingo ya Kizazi, ndiyo inayoongoza kwa kusababisha vifo vyingi zaidi vinavyohusiana na saratani kwa wanawake nchini Tanzania. Jambo la kutia moyo ni kwamba saratani hii inaweza kuzuilika na kutibiwa iwapo itagundulika mapema. Ni jukumu letu kwa pamoja kuunga mkono serikali yetu katika kuongeza uelewa.” Alisema.
Sabi pia alisema kuwa katika miaka miwili iliyopita, mbio za NBC Dodoma Marathon zimekuwa na mafanikio makubwa. “Nina furaha kutangaza kwamba katika miaka miwili iliyopita, mbio hizi zilikusanya zaidi ya Shilingi milioni 300, ambazo zilisaidia kupima wanawake zaidi ya 9,000 ambapo kati yao wanawake 550 waligundulika kuwa na saratani hiyo na hivi sasa wanaendelea na matibabu” alisema.
Post A Comment: