Mkuu wa Mkoa Singida Dk.Binilith Mahenge akizungumza na Wananchi wa Ikungi  mkoani humo katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi uliofanyika viwanja vya Stendi ya Mabasi leo Juni 30, 2022.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi wakipokea kero kutoka kwa mwananchi aliyefika kwenye mkutano huo. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali katika mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi (ACP) Lukas Mwakatundu akizungumza kwenye mkutano huo. 
 Kamanda wa Uhamiaji Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi (ACP) Phaustine  Ngunge akizungumza kwenye mkutano huo. 
Mkutano ukiendelea.
Mkuu Mpya  wa Polisi Wilaya ya Ikungi (OCD) Susan akijitambulisha rasmi katika mkutano huo.

Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.

Mkutano ukiendelea.

Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.

Mhandisi Fred Nkosya kutoka Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Singda akizungumzia mikakati ya ujenzi wa barabara wilaya ya Ikungi.

 Mhandisi wa TANESCO Mkoa wa Singida, Onesy  Mbembe akizungumzia ukamilikaji wa usambazi wa umeme mkoani hapa ambapo alisema hadi kufikia Juni mwakani vijiji vyote vya Mkoa wa Singida vitakuwa vimepata umeme.

Afisa Mfawidhi wa Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) Mkoa wa Singida Layla Daffa akielezea umuhimu wa kudai lisiti kwa abiria jambo litaaaaaakalosaidia kuwabaini wamiliki wa mabasi wanaotoza nauli kinyume na  ile iliyopangwa na Serikali.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Singida, akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa Ardhi Wilaya ya Ikungi, Ambross Ngonyani akielezea mradi wa ujenzi wa Mji Mpya wa Ikungi.

Wananchi wa Ikungi wakiwa wamejipanga foleni tayari kwa kutoa kero zao kwa mkuu wa mkoa.

Mkazi wa Ikungi, Said Kulungu akitoa kero ya ardhi katika mkutano huo.
Mkazi wa Kijiji cha Muungano Juma Omari akitoa kero yake.
Mkazi wa Ikungi, Rebecca Wellia akizungumzia kero yake.
Mkazi wa Ikungi, Masiko Nyagikondo akitoa kero yake.


Na Dotto Mwaibale,  Ikungi


MKUU wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge, amewatahadharisha wananchi kutouza chakula ovyo walichonacho  kwani hali sio nzuri kutokana na maeneo mengi kutopata mvua za kutosha msimu huu na hivyo kupata mavuno kidogo ambayo kama wakiyauza bila mpangilio wataweza kukumbwa na balaa la njaa.

Ametoa tahadhari hiyo leo Juni 30, 2022 wakati akizungumza na wananchi mjini Ikungi ikiwa ni mfululizo wa ziara zake za kusikiliza kero mbalimbali za wananchi katika wilaya zote za mkoa huu na kuzipatia ufumbuzi wa haraka.

Hatua ya Mkuu wa Mkoa kutoa tahadhari hiyo ilifuatia ombi la wananchi wa Kata ya Ikungi kutoa ombi kwa serikali iwapatie chakula cha msaada ambacho kitauzwa kwa bei nafuu kwa kuwa msimu huu wa kilimo hali ya chakula ni mbaya kwani baadhi ya maeneo mazao yamenyauka mashambani hivyo kutokana na ukosefu wa mvua za kutosha.

"Jambo la muhimu ni kupanga matumizi kwenye chakula tulicho nacho, tusiuze ovyo,tunaelewa hali ya mvua haikuwa nzuri na siyo kwa Singida tu ni kwa mikoa yote sasa tunakwenda kupanga foleni kwa nani," alisema.

Dk.Mahenge alisema kutokana na hali hii iliyopo ambayo inaonesha dalili za upungufu wa chakula, wananchi wahakikishe wanalima mazao yanayoweza kustawi maeneo yenye unyevunyevu.
"Ni lazima tujiongeza mwenye kuku afuge, watu wanatoka Dar es Salaam kuja kununua kuku Singida hizo hela ukizipata unanunua mahindi, tusiweke. Matumaini sana kwamba tutaletewa chakula cha msaada," alisema.

Alisema kimsingi hali ya chakula katika dunia sio nzuri kwani hata nchi ambazo huwa tunapata msaada wa chakula nao hakitoshi na hata mafuta ya kula hayawatoshi pia.

"Kule Ulaya wazungu shamba lao anazaliwa anakuwa mkubwa hawajawahi kuwa na ardhi, hawajawahi kuona muhindi wala mgomba duka lake ni 'Super Market' akiingia anakuta kuna magimbi na kila kitu, wao wameishi katika mazingira kama hayo," alisema.

Mkuu wa Mkoa alisema ' super market' ya mtu mweusi (mwafrika) iko shambani hivyo watu wajiongeze maeneo ambako kuna mito kuna maji wapande mazao yanayostahimili maji kidogo kama vile mihogo, viazi vitamu ili kuweza kuokoka na baa la njaa linaloweza kujitokeza.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro, alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa kutokana na wananchi wengi katika wilaya take kutovuna kabisa kukikosabishwa na ukosefu wa mvua, serikali ya wilaya imeanza kufanga tathimini kupata idadi ya wananchi ambao hawana chakula kabisa.

"Ndani ya wiki hii tathimini itakwisha na nitakuandikia barua rasmi ya serikali ya wilaya kuomba msaada wa mkoa ili tujue sisi wilaya tutaoata maasada gani kwenye eneo la chakula.
 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: