Mshauri wa Wanafunzi kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Bi.Analyce Ichwekeleza (kushoto) akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya watoto mahitaji maalum kwa Matroni wa Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Bi. Simphorosa Silalye (Kulia) baada ya kutembelea Hospitali hiyo
Mshauri wa Wanafunzi kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Bi.Analyce Ichwekeleza (kushoto) akieleza jambo wakati wa kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum wa Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru.
Wafanyakazi na Wanafunzi kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela wakiwa wamebeba msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Jijini Arusha Julai 19,2022 Jijini Arusha.
Mshauri wa Wanafunzi kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Bi.Analyce Ichwekeleza (kushoto) akikabidhi msaada wa chakula na vitu mbalimbali kwa Msimamizi wa Kituo cha watoto wa Good Hope Kiwawa Children Home Bw. Eliasante Ombeni (Kulia)mara baada ya kutembelea kituo hicho
Wafanyakazi na Wanafunzi kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha Good Hope Kiwawa Children Home Usariver barabara ya kuelekea Momela mara baada ya kuwatembelea Julai 19, 2022 Jijini Arusha.
Wafanyakazi na Wanafunzi kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha Ikunda kilichopo Maji ya Chai Jijini Arusha mara baada ya kuwatembelea Julai 19,2022 Jijini.
Wafanyakazi na Wanafunzi kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea watoto wenye mahitaji maalum katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Julai 19,2022 Jijini Arusha.
............................................
Na Mwandishi Wetu.
Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela imetoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalum katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru na vituo vya kulelea watoto vya Good Hope na Ikunda vya Jijini Arusha.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Julai 19, 2022 Mshauri wa Wanafunzi kutoka Taasisi hiyo Bi. Analyce Ichwekeleza ameeleza kuwa taasisi hiyo huadhimisha siku ya huduma kwa jamii kwa kutoa misaada mbalimbali ambapo kwa mwaka huu wametoa kadi za Bima ya Afya kwa watoto saba wa vituo vya Good Hope Kiwawa na Ikunda pamoja na vifaa mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji maalumu wa Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru.
"Huwa tunaadhimisha wiki ya Sayansi, Uhandisi,Teknolojia na Ubunifu ya Nelson Mandela kila Julai 18mojawapo ya shughuli ambazo huwa tunazifanya ni pamoja na huduma kwa jamii ikiwemo kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji " amesema Bi. Ichwekeleza
Anazidi kueleza kuwa ni faraja kubwa kuona tabasamu kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wazazi wa watoto wenye mahitaji maalum kupitia misaada hiyo na kutoa wito kwa wadau wengine kuendelea kujitokeza kwa wingi kuweza kusaidia kundi hilo.
Naye Matroni wa Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Bi. Simphorosa Silalye ameishukuru Taasisi Hiyo kwa msaada huo kwa watoto wenye uhitaji maalum na kuomba kuendelea kuwa na moyo huo wa kujitolea kusaidia jamii.
"Tunashukuru kwa msaada huu wa maziwa, nepi (Diapers) na tissue maalum, ni Faraja kubwa kwa wazazi wa hawa watoto "amesema Bi Simphorosa
Aidha Bi. Simphorosa ametoa rai kwa akina mama kuwahi kwenda kliniki ili kuepuka kupata madhara mbalimbali ya afya mara tu pale wanapojigundua kuwa ni wajawazito ili kuweza kupata msaada wa karibu kutoka kwa wahudumu wa Afya.
Kwa upande wake Mwanafunzi kutoka Taasisi hiyo, Bw. Daud Flavian amesema misaada hiyo inagusa jamii moja kwa moja na kutoa rai kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia watu wenye mahitaji maalum ili kuboresha maisha yao.
Post A Comment: