Watanzania wametakiwa kukataa kudanganywa kuhusu zoezi la
sensa kwa sababu ni kitu ambacho kinatambuliwa na dini zote.
"Anayekuambia kuwa dini hairuhusu sensa au ni mambo ya dhambi
anakudanya . hivyo kuanzia leo hadi siku ya sensa mtu asikudanganye
kuhusu sensa," amesema Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Timotheo
Mnzava wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya
maendeleo na kusikiliza kero mbalimbali na kuzitatua,
Mnzava amesema suala la kuhesabiwa ni muhimu sababu Serikali haiwezi
kutengeneza mipango ya maendeleo kwa wananchi wake bila kuwa na takwimu sahihi za wakazi wa eneo husika.
Akitoa mfano wa suala la sensa linavyoyambulika katika dini alisema
kwa Wakristo Yesu alizaliwa katika hori la ng'ombe wakati akienda
Bethlemu kuhesabiwa. Pia litoa hadithi ya Mtume Muhamad (SAW)
ambapoaliema wakati alipokufa aliwaacha waumini na mahalifa wanne.
Abubakari,Omari,Athimani na Ali
Amesema kuwa kati ya mahalifa hao mmoja alipopata malalamiko kuwa
watu hawatendewi sawa aliaimrisha ifanyeike sensa ili ajue idadi
halisi ili watu waweze kuhudumia kwa usawa.
Akifafanua, Mzava alieleza kuwa lengo la sensa hiyo ni kuisadia
Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa
utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya
afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za
kimataifa.
Alisisitiza kuwa taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za
wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi
matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa
mgawanyo wa rasilimali
Katika hatua nyingine Mbunge huyo Alisema ataendelea kuihamasisha
jamii kwenye mikutano ya hadhara na Vikao kwenye ngazi ya Wilaya,
Kata, Vijiji na Vitongoji ambapo aliongeza kuwa watakapopita makarani
wa sensa hakikisheni mnatoa taarifa sahihi bila uoga .
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepanga kufanya Sensa ya
Watu na Makazi ifikapo mwezi Agosti mwka huu.
Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa
kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS),
ipo kwenye maandalizi ya kufanya Sensa hiyo.
Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada
ya miaka 10 ambapo Sensa ya mwisho kufanyika nchini ni ile ya mwaka
2012.
Hivyo Sensa ya mwaka huu itakuwa ni sensa ya Sita kufanyika nchini
baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Sensa nyingine
zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.
Post A Comment: