Meneja wa ukaguzi wa bidhaa zinazotoka nje, TBS Mhandisi Said Issa Mkwawa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Julai 20,2022 katika ofisi za TBS zilizopo jijini Dar es Salaam.
**********************
Shirika la Viwango Tanzania ( TBS) limetoa taarifa kuwa kuanzia Leo Tarehe 20 Julai 2022, magari yote yaliyotumika ( Used Motor Vehicles) yanayotoka nchini Japan yatakuwa yanakaguliwa nchini Japan kabla ya kuja Tanzania kwa utaratibu wa Pre- Shipment Verification on Conformity to Standards ( PVoC)
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za TBS,Meneja wa ukaguzi wa bidhaa zinazotoka nje, TBS Mhandisi Said Issa Mkwawa amesema kuwa ukaguzi magari hayo utafanywa Nchini na Kampuni ya EAA Company Limited ya nchini Japan huku akibainisha kuwa gharama za ukaguzi utakaofanyika ni dola za kimarekani 150 ( zaidi ya ) kwa gari na hakuna ongezeko lolote la gharama za ukaguzi.
Mhandisi Mkwawa ameongeza kuwa utaratibu huo utasaidia kuepuka gharama za matengenezo kwa wanunuaji wa magari.
Amesema Shirika linaendelea na taratibu za kupata mawakala kwa ajili ya ukaguzi wa magari yanayotoka Nchi za Uingereza, Dubai na Singapore na utaratibu huo utakapokamilika basi waingizaji na wafanyabiashara wa magari watapewa taarifa.
Post A Comment: