Mke wa mwanasiasa maarufu nchini na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha TLP,  Augustino Mrema, Doreen Kimbi ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kikundi cha Umoja Shabaha Vicoba uliofanyika mjini Moshi jana.

Mke wa mwanasiasa maarufu nchini na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha TLP,  Augustino Mrema, Doreen Kimbi (katikati) ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwa na Wanaumoja wa kikundi cha Shabaha baada ya kukizindua rasmi. 

Hafla hiyo ikiendelea.
Mke wa mwanasiasa maarufu nchini na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha TLP,  Augustino Mrema, Doreen Kimbi akiwa kwenye hafla hiyo. 

 

Na Thobias Mwanakatwe, MOSHI

 

WANAWAKE nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa ili kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ameonesha dhamira njema katika kuifanya Tanzania kupiga hatua kubwa kwenye nyanja za demokrasia,maendeleo na usawa wa kijinsia.

Wito huo umetolewa jana na Doreen Kimbi ambaye ni mke wa mwanasiasa maarufu nchini na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha TLP,  Augustino Mrema wakati wa hafla ya uzinduzi wa kikundi cha Umoja Shabaha Vicoba uliofanyika mjini Moshi na kuhudhuriwa na wanawake zaidi ya 300.

“Wanawake tumsaidie sana Mheshiniwa Rais kwa kufanya kazi kwa bidii mahali ulipo, kama wewe ni kiongozi kwenye vicoba wajibika kwa kipande chako, kama ni kiongozi kwenye siasa au serikalini wajibika kwa nafasi yako ,”alisema.

Doreen alisema Rais Samia amekuwa akiendelea kufanya mambo makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo kuitangaza nchi kimataifa hivyo ni muhimu sana kwa wanawake kuendelea kumtia nguvu kwa kufanya kazi kwa ufasaha ili nchi yetu iendelee kupaa kimaendeleo.

Alisema wanawake ambao inafahamika ni waaminifu sana na tafiti zinaonyesha hivyo ndio maana katika awamu hii ya sita wengi wamepewa nafasi mbalimbi za uongozi ambazo kimsingi wanazitendea haki.

"Hivi sasa Bunge linaongozwa na mwanamke,taasisi nyingi na nyeti zinaongozwa na wanawake hii ni kwasababu mama (rais) sio mbaguzi anatupeleka wote katika usawa," alisema Doreen.

Aliongozeka kuwa ukiangalia wizara na taasisi zote zinazoendeshwa na wanawake zimekuwa na mafanikio makubwa kimaendeleo sababu ni wachapa kazi na waadilifu.

" Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameanza vizuri kuiongoza nchi na kwa muda wa mfupi akiwa madarakani ametoa mwelekeo chanya wa mustakabari wa Taifa," alisema.

Aidha, Doreen aliwahidi wanawake wa kikundi hicho kutafuta wafadhiri ambao wataweza kukisaidia mitaji ili kiwe na uwezo wa kusaidia wanawake wengi zaidi na hivyo kuinua uchumi wao.

Katika risala yao, wanawake hao walieleza changamoto inayowakabili kuwa mtaji mdogo ambapo waliomba serikali kuwapatiwa mradi wowote wa kuwasadia kuendeleza biashara zao.



 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: