Kelvin Kalumuna, Mkufunzi Msaidizi kutoka chuo cha bahari Dar es Salaam, akitoa huduma Kwa mteja aliyetembelea katika banda la chuo cha bahari Dar es Salaam pamoja na kumsajili Kwa masomo ya msimu wa 2022/2023.
DMI inawakaribisha wananchi wote kufika kwenye Banda lao ndani ya ukumbi wa Nkurumah ili upate taarifa mbalimbali kuhusiana na tasnia ya bahari ikiwa ni pamoja na fursa za masomo na fursa nyingi zitolewazo na chuo cha bahari Dar es Salaam (DMI)
Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) tupo kwenye maonyesho ya46 ya biashara (Sabasaba) katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam
Ukifika katika banda lao utapata taarifa kuhusiana na kozi za ubaharia na namna ya kujiunga lakini pia utafanyiwa usajili wa masomo papo hapo bila gharama yoyote.
Kwa wale ambao watakosa fursa za kutembelea katika banda la chuo cha bahari Dar es Salaam (DMI), wanaweza kutembelea tovuti ya chuo hicho: www.dmi.ac.tz
Post A Comment: