Na,Jusline Marco;Arusha

Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mashimba Ndaki amefungua maonesho ya Karibu Kilifair yanayofanyika jijini Arusha amewakata wananchi kutembelea vivutio vilivyopo nchini.

Akifungua maonesho hayo kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Pindi Chana.Mhe Ndaki  ameihakikishia  dunia kutembelea vivutio vya utalii nchini na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutokana na sekta ya utalii kuwa imefunguka baada ya kupungua janga la Uviko 19.

Aidha amesema kwa sasa masharti yamepungua na maeneo mengi yanafikika kirahisi ambapo pamoja na kuwataka watanzania kutembelea vivutio hivyo pia amewataka wasafirishaji na watoa huduma za utalii kuchangamkia fursa ya uwekezaji katika sekta hiyo.

"Tunatarajia kupitia maonyesho haya kuwa yataiambia dunia,utalii sasa umefufuka tena baada ya kupitia purukushani zile za Corona,sasa kupitia maonyesho haya tunaamini watu wote watajua sasa tunaweza kutembelea Tanzania na EAC,"alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamisheni ya utalii Zanzibar,Rahim Bhaloo,katika maonesho hayo amesema  Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa mazingira rafiki yameshawekwa ikiwemo kuimarisha usalama kwa wageni watakaotembelea nchi hizo.


"Hili linalofanyika hapa tunaunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan hasa katika filamu ya Royal Tour.Hata sisi Zanzibar tumehakikisha usalama wa wageni na hivi karibuni tumeanzisha kikosi kazi cha usalama,"

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Kilifair ambao ndiyo waandaaji wa maonyesho hayo,Dominic Shoo,alisema katika maonyesho hayo zaidi ya washiriki 8,000 wameshiriki.







Share To:

JUSLINE

Post A Comment: