Na; Imma Msumba Arusha
Serikali imepanga kutumia shilingi Trilioni 1.15 katika uboreshaji wa miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa 12000,vifaa vya kujifunzia pamoja na kuwajengea uwezo walimu wa shule za msingi.
Kauli hiyo imetoalewa na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolfu Mkenda wakati akizindua program ya Boost ambapo amesema program hiyo imelenga kuboresha upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora wa elimu ya awali na msingi Tanzania Bara.
Prof.Mkenda amesema mradi huo ambao utatekelezwa kwa Dola za kimarekani milioni 500 sawa na fedha za kitanzania Trilioni 1.15 utaenda kujenga vyumba vya madarasa 3000 kila mwaka ambapo wanatarajia kufikisha vyumba 12000 mwaka 2026 huku mpango wa serikali ukilenga kuimarisha mpango wa mafunzo kwa walimu kazini pamoja na kuziwezesha shile 6000 kutekeleza programu ya shule za msingi.
Aidha amesema progamu hiyo ni muendelezo wa juhudi za Mhe.Rais Samia katika kuboresha sekta ya elimu ambapo kupitia mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19 jumla ya shilingi bilioni 368.9 ziliagizwa kutengwa kwa ajili ya sekta ya elimu katika mpanho huo.
Ameongeza kuwa katika fedha hizo Ofisibya Rais Tamisemi ilipewa jumla ya shilingi bilioni 304 na wizara ya elimu sayansi na teknolojia ilipewa shilingi bilioni 64.9 kwa ajili ya kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu na mafunzo pamoja na kuimarisha mazingira ya ufundishaji.
"Tunamshukuru sana Rais wetu Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa sababu chini ya uongozi wake tunaona sekta ya elimu inapata kipaumbelea cha aina yake,si tu mradi huu wa boost ambao sasa unanlensa kutekeleza lakini pamoja na program zote ambazo ameagiza fedha zielekezwe huko."
Prof.Mkenda amesema program ya Boost inalenga kuimarisha ujifunzaji,kuboresha ujuzi na ubora wa walimu katika ufundishaji sambamba na kuimarisha upatikanaji wa rasilimali za kuwezesha utoaji wa huduma katika ngazi za halmashauri.
Vilevile amesema kuwa program ya mradi wa boost itajikita katika afua mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya shule za msingi kwa kuzingatia majitaji muhimu ikiwemo ujenzi wa madarasa ,uimarishaji wa mpango wa shule salama pamoja na uimarishaji wa uwiamo wa uandikishwaji wa wanafunzi wa elimu ya awali.
Kwa upande wake Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.David Silinde ameipongeza serikali kwa kudhamiria kuiboresha sekta ya elimu kipitia mradi huo ambao unatokana na fedha za mkopi wenye riba nafuu kutoka katika Benki ya Dunia.
Naye Mwakilishi wa Benki ya Dunia Nchini Tanzania Miss Mara Warwick katika hafla hiyo amesema kuwa zaidi ya watoto milioni 12 wanatarajiwa kunufaika na mradi huo wa Boost ambao unalenga kuboresha elimu ya awali nchini.
Kamishna wa Elimu Wizara ya elimu sayansi na teknolojia Dkt.Lyambwene Mtahabwa amesema uboreshaji wa elimu kupitia mradi wa Boost utasaidia kukuza ubora wa elimu ya awali.
Post A Comment: