Waziri wa elimu ,sayansi na Teknolojia ,Prof .Adolf Mkenda amezindua mradi wa kuboresha upatikanaji wa fursa sawa katika utunzaji bora wa elimu ya awali na msingi Tanzania bara (Boost) utakaogharimu tatribani shs Trilioni 1.15 .
Aidha mradi huo ambao unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano unalenga kuimarisha sekta ya elimu nchini hususani katika maswala ya miundombinu .
Prof.Mkenda akizungumza katika uzinduzi wa programu hiyo, amesema mradi huo umefadhiliwa na benki ya dunia kwa lengo kuhimarisha nyanja mbalimbali katika sekta ya elimu kuanzia ngazi ya elimu ya awali.
“Mradi huu unatarajiwa kutoa matokeo muhimu na kuimarisha mfumo wetu wa elimu katika ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa 12,000 na vifaa vya shule vinavyohusika katika maeneo yenye uhitaji zaidi,”amesema Waziri Mkenda.
Pia amesema matokeo mengine ni pamoja na kuanzishwa kwa vituo vya walimu na kuendelezwa kwa ajili ya utoaji wa mafunzo kwa njia ya TEHAMA kupitia maktaba mtandao,shule za msingi 6000 kuwezeshwa kutekeleza programu za shule msingi salama.
“Mradi huu utasaidia kuongezeka kwa uwiano wa uandikishwaji wa wanafunzi wa elimu ya awali kutoka asilimia 76.9 hadi 85 pamoja na kuongeza kiwango cha wanafunzi kubaki shuleni katika halmashauri zilizo katika kundi la robo ya chini kutoka asilimia 55.9 hadi 66.2,”amesema Prof.Mkenda.
Kamishna wa elimu Tanzania Dk.Lyabwene Mtahabwa amesema mradi huu unajenga watoto kuanzia ngazi ya shule ya awali hivyo serikali imeamua kutumia mbinu ya kurekebisha hali ya kukabiliana na ufisadi na kuweza kuwa mzalendo katika nchi yake.
Dkt.Mtahabwa amesema programu ya boost ni mpango wa lipa kulingana na matokeo katika elimu yaani (EPforR II) ikiwa maandalizi ya utekelezaji yameshakamilika kutokana na majadiliano mbalimbali kati ya serikali na Benki ya dunia katika uendeshaji wake.
“Programu hii ya boost imetokana na changamoto zilizobainika katika uchambuzi wa taarifa za sekta ya elimu ya mwaka 2021 ambazo zinaathiri utoaji wa elimu bora kwenye ngazi ya elimu msingi,”amesema.
Amesema kuwa, baadhi ya changamoto hizo ni kuwepo kwa msongamano wa wanafunzi madarasani kutokana na uhaba wa miundombinu wa madarasa,baadhi ya shule kutokuwa na mazingira rafiki ya ujifunzaji na ukosefu wa vifaa vya ufundishaji wa elimu ya awali.
Mkurugenzi mkaazi wa benki ya dunia,Mara Warwick amesema mradi huu unaongeza nafasi ya watoto wengi kupata elimu ya awali na msingi pamoja na kuongeza ushindani wa uwajibikaji kwa walimu.
“Mradi huu utawanufaisha zaidi ya wanafunzi milioni 12 hivya naiomba serikali ya Tanzania kuondoa baadhi ya vikwazo vinavyozuia watoto kushindwa kupata elimu msingi,”amesema Warwick.
Post A Comment: