Na John Mapepele
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amekutana na
msanii nguli kutoka Nigeria Jim Iyke na kufanya mazungumzo ya
mashirikiano katika kuandaa filamu za kimkakati za pamoja baina ya
Tanzania na Nigeria
Mazungumzo
haya yamefanyika leo Juni 14, 2022 jijini Dodoma ambapo wamekubaliana
kuwa na mashirikiano kwenye filamu za kimkakati kwa faida za pande
zote mbili.
Aidha, Mhe.
Mchengerwa amesema mashirikiano hayo yataifanya Tanzania kunufaika zaidi
kwa kufanya kazi na manguli wa filamu wa Nigeria ambao wanawapenzi
wengi duniani.
Waziri Mchengerwa ametumia fursa hiyo kuwakaribisha watu mbalimbali duniani kuja kuwekeza kwenye sekta ya Sanaa na Michezo.
Post A Comment: