Na Ahmed Mahmoud
Shirika la uwakala wa Meli Tanzania’TASAC’ Iimeeleza kwamba licha ya muitikio na utekelezaji wa maagizo mbalimbali yanatolewa kwa wasifiri wa majini bado kuna changamoto kadhaa hali ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya watu .
Hayo yameelezwa na afisa mfawidhi kutoka shirika la uwakala wa Meli Tanzania mkoa wa Tanga ‘TASAC’ kapten Christopher Shalua wakati akiwa katika maonyesho ya 9 ya utalii na biashara yanayofanyika mkoani Tanga na ambapo shirika hilo linaelekeza na kutoa katazo kwa wamiliki wa vyombo vya kusafirisha abiria kutokutumia kusafirisha binadamu kutoka sehemu moja kwenda nyingine ili kuweza kuepukana na athari ambazo zinaweza kujitokeza na hatimaye kughalimu maisha ya binadamu.
Ameongeza kuwa wamekuwa wakizitumia kamati za ulinzi na usalama kudhibiti bandari bubu ambazo zimekuwa zikitumika kusafirisha abiria pamoja na mizigo kwa njia zisizo rasmi na kuwashirikisha viongozi wa serikali za mitaa ili kuhakikisha wanashirikiana katika kudhibiti abiria kutumia vifaa ambavyo havijaruhusiwa.
Nae Afisa Uhusiano mwandamizi kutoka shirika hilo Amina Miluko amebainisha kwa kuzingatia majukumu yao wamekuwa wakiwafuatilia bandari zote hapa nchini ikiwemo bandari kavu kwa lengo la kuhakikisha usalama wa raia na kudhibiti mianya yote ya usafirishaji unaokiuka sheria.
Aidha amewataka wananchi pamoja na wamiliki wa vyombo vyote vya usafirishaji wa mizigo pamoja na abiria kufuata sheria za usafirishaji hapa nchini sambamba na kurasimisha bandari zote bubu.
“Kikubwa tunachokifanya ni kuendelea kushirikiana na mamlaka ya bandari hapa nchini kutoa elimu kwa wananchi pamoja na wamiliki wa vyombo ambapo ni pamoja na kukagua vyombo vyote vinavyotumika kwa kupanga au kustukiza na kuhakikisha kuwa bandari zote bubu zilizopo zinafuata sheria kwa kurasimishwa” amesema Mwiluko.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adamu Malima akipata Maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa TASAC Amina Miluko katika Banda la shirika hilo katika maonesho ya Utalii yanayoendelea Jijini Tanga picha zote na Ahmed Mahmoud
Post A Comment: