Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dk. Batilda Burian akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki ya Exim kwa ajili ya wateja wadogo na wakubwa wa Mkoani Tabora hivi karibuni ili kujadili fursa za biashara na kutambulisha huduma mpya za benki hiyo.


Mkuu wa Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, Bw Paul Chacha akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki ya Exim kwa ajili ya wateja wadogo na wakubwa wa Mkoani Tabora hivi karibuni ili kujadili fursa za biashara na kutambulisha huduma mpya za benki hiyo.




Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo (Kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dk. Batilda Burian wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo mwishoni mwa wiki kwa ajili ya wateja wadogo na wakubwa wa mkoani humo ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo




Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wadogo na wakubwa wa Mkoani Tabora hivi karibuni ili kujadili fursa za biashara na kutambulisha huduma mpya za benki hiyo.




Viongozi waandamizi wa Benki ya Exim wakiwa pamoja na wageni waalikwa ambao ni wateja wa benki hiyo Mkoani Tabora akiwemo Mkuu wa Mkoa huo Balozi Dk. Batilda Burian kwenye hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wadogo na wakubwa wa mkoani Tabora ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo.




Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dk. Batilda Burian (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, Bw Paul Chacha wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya Exim wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wadogo na wakubwa wa mkoani Tabora ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo.


...............................................


Na Mwandishi Wetu-Tabora


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dk. Batilda Burian amewaomba wafanyabiashara mkoani humo kuhakikisha wanachangamkia vema uwepo wa taasisi za kifedha ikiwemo Benki ya Exim mkoani humo kwa kufanya uwekezaji katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi ili kuuendeleza mkoa huo.


Akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki ya Exim kwa ajili ya wateja wadogo na wakubwa wa mkoani humo mwishoni mwa wiki iliyolenga kujadili fursa za biashara na kutambulisha huduma mpya za benki hiyo Balozi Dk. Burian alisema bado wakazi wa mkoa huo hawajaweza kutumia kikamilifu uwepo wa taasisi hizo katika kujikwamua kiuchumi wao binafsi na faida ya mkoa kwa ujumla.


“Mkoa wa Tabora upo kwenye uchumi unaokua. Ili kufanikisha ukuaji wake tunahitaji sana wawekezaji kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji na viwanda ili kukchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wetu. Ni sisi kama wana Tabora ndio tuna jukumu hilo tusisubiri watu watoke mikoa mingine kuja kufanya jambo hilo hapa. Na benki ya Exim wapo hapa leo kutukumbusha hilo hivyo nachoomba ni ushirikiano wenu mchangamkie huduma zao ikiwemo mikopo,’’ alisema.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kaliua mkoani humo, Bw Paul Chacha alisema kupitia huduma ya Exim Wakala wakazi wa mkoa huo wanatarajia kuchangamkia zaidi huduma za kifedha kupitia benki hiyo kwa kuwa hapo awali walishindwa kufanya hivyo kutokana na wananchi katika maeneo mengi kushindwa kufikiwa na huduma za benki hiyo.


“Mwaka huu tunatarajia kuvuna tumbaku kiasi cha zaidi ya kilogram milioni 10 hivyo tunatarajia huduma nzuri pia za kifedha. Ujio wa Exim Wakala utakuwa ni mkombozi kwa wananchi wa Tabora ambao licha ya kuvutiwa na huduma za Exim muda mwingine wamekuwa wakishindwa kuitumia vema benki hii kwa kuwa walikuwa hawafikiwa na huduma zake kwa ukaribu zaidi.,’’ alisema.


Awali wakizungumza kwenye hiyo, Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo alisema benki kwa sasa inauweka mkoa wa Tabora katika vipaumbele vyake kwa kuhakikisha zaidi huduma zake katika mkoa huo zinakwenda sambamba na mkakati wa mapinduzi ya kiuchumi ya mkoa huo.


“Tumebaini kwamba kwasasa mkoa wa Tabora unapitia mabadiliko makubwa ya kiuchumi katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara na kilimo ambayo yanahitaji ushiriki mkubwa wa taasisi za kifedha na hivyo benki ya Exim tupo tayari kwa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha hilo. Ujio wa huduma yetu ya Exim Wakala unalenga kufanisha hilo zaidi hivyo tunaomba sana wana Tabora mtupokee,’’ alisema Bw Lyimo.


Kwa upande wao baadhi wa wafanyabiashara mkoa huo walisema wakati mkoa huo ukiwa unajipanga kujenga uchumi imara na endelevu, ufanisi katika mfumo wa fedha ni moja ya mahitaji ya muhimu kwao ili waweze kushiriki katika katika ukuaji wa uchumi huo na maendeleo kwa ujumla.


“Ndio maana leo tumeshukuru sana kuona Benki ya Exim imetuita hapa kututangazia kwamba ipo pamoja na sisi katika kufanikisha hili. Tunawashukuru sana kwa hilo na sisi tupo tayari watupokee’’ alisema Bw Snega Juma mmoja wa wafanyabiashara mkoani humo.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: